Breaking

Saturday, February 15, 2020

Mambo Yatakayomfanya Mwanamke Asitoke nje ya Ndoa


Mapenzi yana kanuni zake, kanuni ambazo usipozifuata huwezi kupata furaha uliyotarajia. Unapotokea kumpenda mtu, hiyo ni hatua ya kwanza lakini omba sana upate ile bahati ya kumpenda mtu ambaye naye anakupenda kwa dhati.

Kwa bahati mbaya ukitokea kumzimikia mtu ambaye wala hana hata chembe za penzi kwako, utaumia sana na kama utalazimisha kuwa naye, utakuwa unajitafutia vidonda vya tumbo.

Hata hivyo, wapo waliobahatika kuwapata wapenzi wa ukweli lakini kwa kushindwa kwao kujua yapi ya kufanya ili kudumisha penzi, leo hii wameachika na bado wanaranda mtaani.

Kwa kifupi ni kwamba, unapoingia kwenye uhusiano na mtu na ukabaini naye anakupenda, hutakiwi kubweteka bali unatakiwa kutumia utundu na ubunifu wako katika yale ambayo yatamfanya huyo mtu wako ahisi wewe ni wa pekee kwake.

Ninapozungumzia hayo, namaanisha ubunifu kwenye mambo mengi ambayo hakika nikianza kuyaelezea hapa, nafasi inaweza isitoshe ila kwa leo nigusie utundu katika uwanja wetu ulee wa kujidai.

Faragha ni eneo muhimu sana ambalo linaweza kubomoa au kuimarisha ndoa. Ninapozungumzia hilo, ni kwa wote yaani mke na mume.

Mwanaume anatakiwa kumridhisha mkewe kwa kiwango kinachostahili. Kusiwepo mazingira ya kupeana mambo kiduchu kwani ikiwa hivyo lazima mke atakosa furaha iliyokamilika.

Ila sasa leo nataka niwazungumzie kwa kirefu wanawake. Kuna wanawake ambao wamebahatika kupata wanaume wanaowapenda sana na kuwapatia kila wanachohitaji.

Hawa wanatakiwa kujiona ni wenye bahati kubwa kwani kwa hali ilivyo sasa, wanawake wengi wanatafuta wanaume wa kuwaoa hawawapati.

Kinachonishangaza ni kwamba, kuna baadhi ya wanawake ambao wako ndani ya ndoa lakini wamejisahau kwamba wana jukumu la kuwapa waume zao furaha ambazo hawawezi kuzipata kwingine.

Ukijaribu kuchunguza utabaini wanawake wengi walio ndani ya ndoa siku hizi wanasalitiwa sana. Hii ni kwa sababu wamekuwa waongeaji sana lakini wanapokuwa faragha unaweza ukadhani siyo wao. Hawajui kitu, wamekaa kama magogo tu halafu eti wanadhani hawatasalitiwa na ndoa zao zitadumu, zitadumu kwa misingi ipi?

Mwanamke akae akijua kwamba, mumewe ni kama mtoto ambaye anatakiwa kubembelezwa huku akipewa vitu vitamu ili kumpumbaza asishawishike kutoka nje. Ukiwa kwenye ndoa kisha ukachukulia kila kitu poa tu eti kwa kuwa tayari ulishapendwa ipo siku utajikuta ni mke wa pambo la nyumba tu.

Mtaani kuna utitiri wa nyumba ndogo, wanaume walioanzisha makoloni hayo nje ya ndoa zao walikosa wake sahihi ambao wanaweza kuwashikilia waume zao.

Matokeo yake sasa nyumba ndogo hizo ndizo zinazoonekana kuwashika waume za watu siku hizi na wanafanikiwa kwa kuwa ni watundu na wabunifu.

Sasa kwa nini wewe mwanamke uliye ndani ya ndoa usifanye kama yale wanayofanya nyumba ndogo? Kuna dada mmoja nilizungumza naye hivi karibuni akaniambia eti amenuniana na mumewe huu ni mwezi wa pili baada ya mwanaume wake huyo kutaka afanyiwe mambo ambayo yeye aliona kinyaa kuyafanya.

Kabla ya kumjibu kwanza niliguna, sababu ya kuguna ni kwamba niliyagundua hayo mambo ambayo aliona kinyaa kumfanyia mumewe. Niseme tu kwamba, mapenzi wakati mwingine ni uchafu, wanaojua mapenzi wanajua kwa nini nasema hivyo.

Nilichomjibu mwanamke huyo ni kwamba, kama mwanaume huyo anampenda amfanyie kila atakacho isipokuwa kukubali kufanya mapenzi kinyume na maumbile na nikamwambia kuwa, mapenzi ni uchafu hivyo hayo ambayo anaona kinyaa kumfanyia mumewe ndiyo ambayo wengine wamekuwa wakiyafanya na wamefanikiwa kuzishika ndoa zao.

Naomba niseme tu kwamba, huenda unajiamini kuwa ni mzuri na umbo la kuvutia kiasi kwamba, ni rahisi kupata mwanaume wa kuoa lakini tambua bado utakuwa na kazi kwenye kuidumisha ndoa na kuhakikisha hukaribishi mazingira ya mumeo kutafuta nyumba ndogo.

Hakikisha unaonesha uanamke wako ili hata kama huyo mumeo atatoka nje, iwe ni kwa tamaa zake tu lakini mambo ya msingi uwe unampatilizia.

No comments:

Post a Comment