Breaking

Thursday, February 6, 2020

Mashabiki Walipwa TZS 722,000 Baada ya Ronaldo Kukosa Mechi
Baada ya Mchezaji maarufu wa mpira Cristiano Ronaldo kukosa mechi ya kirafiki, Mahakama moja nchini Korea Kusini imeagiza mashabiki wawili kulipwa fidia ya £240 (Sawa na Tsh. 721,727.50)

Waandaaji wa mechi hiyo, The Fasta wametakiwa kulipa fedha hizo baada ya kutangaza kuwa Ronaldo atacheza kwa dakika 45 dhidi ya Ligi ya K, Julai 2019. Lakini tofauti na ilivyotarajiwa, mchezaji huyo hakutokea

Wakili Kim Min-ki amesema mashabiki hao walipata Shinikizo la kiakili, na kudai waandaaji walidanganya kwa maslahi yao wenyewe

Tiketi 65,000 ziliuzwa ndani ya dakika tatu baada ya mashabiki kuahidiwa kuwa Ronaldo atakuwepo katika mechi hiyo

Ilipogundulika kuwa mchezaji huyo hatocheza, mashabiki walikasirika na kuanza kuimba nyimbo za kumsifia Mchezaji wa Barcelona, Lionel Messi

No comments:

Post a Comment