Breaking

Monday, February 3, 2020

Meneja akanusha kifo cha Meja Kunta, aomba radhi watanzania

Taarifa mpya ambazo zimetoka kwa mtu ambaye alikuwa kwenye safari moja na msanii Meja Kunta, aitwaye Wasowiso amekanusha taarifa zilizokuwa zikieleza kuhusu kifo cha Meja Kunta, ambapo amesema ni mzima na anaendelea vizuri.

Kupitia ukurasa wa mtandao wa Instagram wa Wasowiso amepost picha ya Meja Kunta kisha ameandika "Habari zinazoendelea mitandao sio za ukweli Meja Kunta anaendelea vizuri mzima kabisa".

Aidha kwa upande wa meneja wa msanii huyo aitwaye G Maker, ambaye alitoa taarifa za kufariki kwa msanii huyo ameomba msamaha kwa kutoa taarifa hizo kupitia mtandao wa Instagram ambapo ameandika.

"Ndugu Watanzania, mashabiki wa mziki wa singeli na mziki kwa ujumla, Wazazi, Waandishi wa wa Habari, ndugu jamaa na marafiki, nasikitika au kuomba radhi kwa nilichokiandika jana usiku kupitia ukurasa wangu wa instagram, Meja Kunta ni mzima wa afya nipende kuwatoa hofu, naomba sababu ya post niiongelee wakati mwingine. kwa dhati kabsa naomba samahani tena" ameandika G Maker


No comments:

Post a Comment