Breaking

Monday, February 17, 2020

Mondi, Tanasha Tutawambia Nini Watu?


TUTAAMBIA nini watu? Ndiyo msemo unaotumika huko mitandaoni baada ya staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ kurejesha mapenzi shatashata kwa mzazi mwenzake, Tanasha Donna.

Penzi la Diamond au Mondi na Tanasha linadaiwa kukumbana na misukosuko, lakini Ijumaa iliyopita (Valentine’s Day), mambo yalirudi kwenye mstari ambapo wawili hao walionekana wakijiachia kimahaba huko Nairobi nchini Kenya.

Mondi anaonekana kufanya juhudi za hali ya juu kutuliza hali ya hewa kwa kumuonesha Tanasha mahaba ya kiwango cha juu.

Moja ya kauli za Mondi juu ya mapenzi ni kwamba anaamini katika kutoa zawadi kwa wanawake na ndivyo ambavyo amekuwa akifanya kwa wapenzi wake ili kuonesha ni kwa kiasi gani anavyowapenda akina mama kwenye maisha yake.

Achana na aliowanunulia magari na zawadi nyingine za kuhamishika, lakini moja ya zawadi kubwa aliyowahi kutoa kwa mpenzi wake ni ile ya kumnunulia Zari (Zarinah Hassan) zawadi ya nyumba nchini Afrika Kusini wakati wa penzi lao.

Sasa, katika kuonesha kwake mahaba kwa Tanasha, Ijumaa iliyopita, Mondi alimtoa ‘auti’ mwanamama huyo na kwenda naye kwenye chakula cha usiku (dinner) kwenye hoteli ya kifahari huko Ziwa Naivasha, Nakuru nchini Kenya.

Hata hivyo, wananzengo hasa kutoka ‘kambi’ ya Zari, wanadai kuwa Tanasha hajamfikia mwanamama huyo wakidai angepewa hata nyumba naye asuuzike roho.

Wakati hayo yakitokea, Mondi alikuwa nchini Kenya kwa ajili ya shoo ya Koroga Festival, lakini aliona siku hiyo (Valentine’s Day) isipite bila kufanya kitu spesho kwa mama huyo wa mtoto wake, Naseeb JR.

Baada ya tukio hilo, wawili hao waliachia mapicha kama yote kwenye kurasa zao za mitandao ya kijamii na kuzima zile kelele za kuachana.

Kwa upande wake, Tanasha amemshukuru Mondi kwa namna alivyomjali na kuonesha mahaba mubashara, huku akiwasisitiza mashabiki wake kuonesha upendo wa kweli kwa wenzao.

“Asante mpenzi wangu kwa usiku huu maalum, ninawatakia Valentine’s Day njema kwenu nyote.

“Tukumbuke kuwapenda wenzetu kila siku na siyo leo tu,” aliandika Tanasha.

Mwaka jana, siku kama hiyo (Valentine’s Day) Mondi alimpelekea Tanasha maua pamoja na zawadi nyingine ndogondogo akiwa kazini alipokuwa mtangazaji wa Radio NRG ya Mombasa nchini Kenya.

Wakati huo, Tanasha alikuwa mtangazaji kwenye redio ya NRG, lakini sasa ameacha kazi hiyo na kujikita kwenye muziki.

Wiki mbili zilizopita, penzi la Mondi na Tanasha lilidaiwa kuwa chumba cha mahututi likipumulia mashine, ambapo mashabiki wengi walisubiria kuona Valentine’s Day itakuwaje?

Akizungumza na gazeti hili wiki iliyopita, Tanasha alikanusha madai yaliyosambaa kuwa ameachana na Mondi na kwamba walikuwa wanaendelea vizuri.

No comments:

Post a Comment