Breaking

Friday, February 14, 2020

Soma Kisa Hichi Kilichomkuta Huyu Baba Baada ya Simu Kuita Bahati Mbaya Akiwa Kanisani


Simu yake iliita kwa Bahati mbaya wakati wa ibada akiwa kanisani 📞☎

Mchungaji alimfokea

Waumini walimzonga baada ya maombi ya ibada
Wakati anarudi nyumbani, njia nzima mkewe aliendelea kumsema kwa kutokuwa makini
Akajisikia vibaya sana, huzuni, na aibu juu

Jioni yake, ili kupoteza mawazo, alikwenda bar

Aliagiza bia, akaiweka mezani. Kwa kuwa alikuwa na mawazo mengi, akaigusa pombe ikamwagika 🍻🍺

Muhudumu alikuja, akampa pole kwa unyenyekevu, na akafuta meza kiustaarabu, kisha akamfuta jamaa ilipommwagikia kiunyenyekevu

Meneja wa bar ile alimpa jamaa bia ya ofa kufidia iliyomwagika 🥂🥃🍾
Muhudumu wa kaunta alipomletea alim'busu akim'bembeleza, "Usijali, hakuna ambaye hana makosa!"

Jamaa hajawahi kukosa 'ibada' ktk bar hiyo tangu siku ile

SOMO:
Unavyowatendea watu kunaweza kujenga au kuwabomoa, hasa wanapokosea

No comments:

Post a Comment