Breaking

Thursday, February 6, 2020

UTAMU WA MAMA Sehemu Ya 1

MTUNZI: GODFREY GODSTAR

CONTACT: 0712730692

FB PAGE: Godstar_tz

PARTY 1.

Pilikapilika za hapa na pale zikiwa zimepamba moto katika wilaya ya tandahimba,jasho likiwa linawatiririka baadhi ya vijana kutokana na Nazi ngumu walizokuwa wanazifanya pamoja na jua la utosi lililokuwa linawaka kwa muda huo,kama kawaida kwenye mkusanyiko na msongamano wa watu wengi huwa hapakosi shughuli mbalimbali za biashara na zakawaida,sauti za minada zilikuwa zilikuwa zikirindima kwa wakati huo na ukizingatia gulio la siku hiyo lilikuwa limepamba moto kisawasawa,upande huu wakipaza sauti za kunadi nguo na wengine wananadi vyombo,huku wananadi samaki na kule wakipiga mnada wa vifaa vya umeme ilimradi tu kila mmoja anauza na kununua akipendacho.
Tandahimba ni wilaya ambayo imechangamka sana kati ya wilaya zilizopo katika mkoa wa mtwara,wenyeji wa wilaya hii waliipamba sana na kutokana na ufanyaji wao Wa kazi huku wakiamini kwamba kilimo ndio jambo la msingi na ndio kinaweza kuwaletea mafanikio katika maisha yao,wageni mbalimbali wa makabila tofauti wapo hapo waliokuja kwa ajili ya kuleta biashara hasa katika kipindi hiki cha msimu wa korosho,wapo walioamua kuhamia hapo hapo na kuwa makazi yao ya kudumu,wakaoa na kuolewa,mmakonde akamuoa mzaramo,mdigo akamuoa mmakonde huku umoja na ushirikiano ukiwa umedumishwa kwa wenyeji pamoja na wageni,utamaduni pia ulidumishwa sio kwa tandahimba tu kwa mkoa mzima wa mtwara,vijana walifanyiwa unyago huku ngoma mbalimbali zikivumishwa ukiachana na singenge tu,palikuwa na chingenge,lingwalangwanja n.k

Yapata saa 12 jioni nikuwa njiani naelekea nyumbani huku miguu yangu ikiwa chakavu kutokana na vumbi nililolibeba nikiwa mpilani lakini pia mwili ukiwa umejawa na uchovu wa kurupushani za hapa na pale nikiwa ndani ya uwanja,nikikata mapori na mashamba ya mikorosho iliyopo mnyawa nikielekea mchichira.
umbali ulipo kati ya mnyawa na kijiji cha mchichira sio mbali hivyo sikuchelewa sana kufika nyumbani,wakati uvivu wa mwendo niliotembea unanipelekea niingie ndani moja kwa moja na kuketi katika kitanda changu cha Namba ambacho ndio sehemu yangu ya kuegesha na kunyoosha mbavu zangu,huku nikiwa na mawazo kibao kichwani mwangu nikitafakari juu ya hatma ya maisha yangu,juu ya wazazi wangu ambao yangu nizaliwe na kupata akili sijawahi kuwaona walaa kusikia kama wapo ingawa maneno ya hapa na pale ninayiyasikia mitaani wengine wakiniambia kwamba wamefariki na wengine wakisema bado wapo ila mwenye ukweli zaidi juu ya wazazi wangu na yeye nikimuuliza ananiweka kwenye mabado hanipia majibu ya kueleweka,nabaki najiuliza ni nani asiyetamani kuishi au kukaa na wazazi wake,furaha kwangu imekuwa kitendawili au methali zinanenwa lakini hazionekani lakini huzuni imekuwa ndio rafiki wa maisha yangu huku machozi ni kama mvua ila mvua isiyokuwa na kipindi maalumu maana sio masika wala kiangazi yanatiririka tu katika mashavu yangu.
nikiwa bado nimeshika tama mawazo yakiwa yamejaa kichwani nilisikia sauti ya babu ikiniita na kunifanya nitoke katika msongo wa mawazo na moja kwa moja nilinyanyuka kitandani na kuelekea nje alipo babu.
"vipi MASUMBUKO mbona umechelewa kurudi leo mjukuu wangu"
babu aliniuliza hilo swali baada tu ya kusalimiana naye ila nilimjibu kwamba nilikuwa mpirani kijiji cha pili na sikuchukuwa baiskeli leo hivyo nimetembea kwa mguu babau,
jibu langu lilimfanya aridhike mzee na kuniambia kama haujala nenda ndani kwangu ukachukue mihogo na mamung'unya ila kutokana nilikotoka nilipitia kwa rafiki yangu nikala hivyo sikuwa na budi kumwambia kwamba nimeshakula na nimeshiba.

"sawa mjuu kuu wangu kama umeshakula acha nikuache ukapumzike na ujiandae kwa ajili ya majukumu yako ya kishule kesho si unajua kesho ni juma tatu"

baada ya kuniambia hivyo babu aligeuza na kuelekea kwakwe lakini kabla hajafika mbali nimuita na yeye bila ajizi aliitikia with wangu na kusimama na Mimi nikapiga hatua kumfuata aliposimama.

"nakusikiliza MASUMBUKO mjuu kuu wangu sema unatatizo gani"

babu baada ya kumfuata aliniambia hayo bila ya hofu nikashusha pumzi kwanza huku ndani ya moyo nikisema liwalo na liwe tu kweli ni babu yangu ila kwa sasa yeye ndio baba na yeye ndio mama ila ukweli anao yeye,nilimtazama usoni kisha nikamuuliza haya

Mzee limo Mimi ni nani kwako?

baada ya kumuuliza swali hilo alishindwa kunijibu akajifanya yesu na kunipachika swali juu ya swali,

"kwanini umeniuliza hivyo mjukuu wangu"

babu hakuna swali linaloulizwa alafu likapachikwa swali Bali swali hupatiwa jibu kwanza alafu ndio upandikizwa swali, naomba unipe jibu la swali nililokuuliza Mimi ni nani kwako?

babu alinitazama sana usoni huku kichwani chache nikiwa kinatafakari nimepatwa na tatizo gani Leo basi akanijibu kwa mkato t,

"Mimi ni babu yako na wewe ni mjukuu wangu mtoto wa mwanangu KAZUMARI"

jibu la babu ndio lilikuwa shida yangu maana naamini jibu lake ndio linaweza likazaa maswali yaliyopo kichwani mwangu na kutimiza hatma ya ninachokitaka,

babu naamini hakuna mtoto hasiye na mama wala mtoto hasiye na baba,na bahati ya kuzaliwa pasipo na baba aliipata yesu peke yake ila si kwa wanadamu wa kizazi hiki cha muhammad,babu furaha ndio hitaji la moto wangu laiti machozi yangekuwa ni juwisi au asali basi babu Leo hii Mimi ningekuwa tajiri,kila siku nakuambia nieleze wazazi wangu wapo wapi,wamekufa au wanaishi na kama wamekufa makaburi yao yapo wapi nikadhuru na kama wanaishi wapo maeneo gani nikawatafube babu yangu.

babu alibaki aknitazama kwa huruma na hofu baada ya kumueleza hayo na kumuuliza hill swali,

"MASUMBUKO jambo jema mjukuu wangu haliitaji haraka amini niyanenayo wala hawajafa kwa kumbukumbu zangu na ipo siku utaujua ukweli wote,sipendi unavyosononeka ingawa pia sipendi unavyoniuliza hayo maswali maana unanupa uchungu usiotaka maji take"

babu alinifuata akanifuta machozi na kuniambia niende ndani nisihofu,akaamua kuelekea kwakwe ila alipofika mbele aligeuka na kutabasamu,tabasamu ambalo lilinifanya nijiulize kwanini babu anatabasamu,kunajambo gani la kumfanya atabasamu juu ya haya niliyomueleza au ananificha nini?

HUSIKOSE PARTY 2

MBELE NDIO KUTAMU KWENYE MAHABA NA RAHA YA KITANDA ILA NAKUSII KAMA HAUNA MPENZI HUKO MBELE HAKUKUFAI KUSOMA MAANA NI SEX BILA MAUMIVU.Image may contain: 1 person, sitting and text

No comments:

Post a Comment