Breaking

Sunday, February 9, 2020

UTAMU WA MAMA Sehemu Ya 10

MTUNZI: GODFREY GODSTAR
CONTACT: 0712730692
FB PAGE: Godstar_tz
SEHEMU YA 10
ILIPOISHIA
kitendo cha madame vero kuniambia vile ndio kimfanya angel.....
ENDELEA NAYO
angel aligeuka na kunitazama na mimi nikajifanya kuzuga nikatoka haraka haraka na kuelekea bafuni kuoga na wala sikukawia hivuo nilitoka.
mishale ya saa 12 asubuhi tulifika shuleni nikiwa na madame hivyo niliteremka kwenye gari na kuchikua mizigo yake nikampelekea moja kwa moja ofisini kwake,wakati natoka ofisini kwa madame vero uso kwa uso nilikutana na swaumu huku akiwa ananitazama kwa jicho la hasira sana.
"hivi masumbuko ni wapi nilipokukosea jamani,wewe ni mwanaume gani husiojuwa nini maana ya kupendwa unataka nikupe nini au unataka nikupe nyum ili ujue kwamba nakupenda"
wakati swaumu akiwa anayaongea hayo nilibaki nikimtazama huku machozi yakimtoka kitendo ambacho kilinifanya nijawe na huruma hivyo nilimwambia afute machozi tu na asilie pale ni shule na akumbuke tumekuja kusoma.
basi swaumu bila kubisha alifanya nilivyomwambia na muda huo kengere ya kuingia darasani iligonga,masomo siku hiyo yalienda vizuri kwa wenzangu ila kwangu ilikuwa tofauti maana nilikuwa namfikiria sana swaumu juu ya maneno aliyokuwa ananiambia na sikujua kimemsibu nini,wakati nikiwa bado nipo kwenye mawazo kuna mwanafunzi alikuja mbiombio darasani kwetu huku akihema.
"oooohp masumbuko,masumbuko fanya haraka mwalimu mkuu anakuita"
kwakweli ule ujaji a aliokuja nao na jinsi anavyoniita nilipatwa na hofu huku nikijiuliza nimefanya kosa gani tena,basi nilinyanyuka haraka haraka na kuelekea ofisini kwa mwalimu mkuu ila nilipofika kule nilistaajabu kumkuta swaumu tena akiwa analia sana,nilimwamkia mwalimu,
"masumbuko nimekuita hapa nahitaji msaada wako"dada mkuu anaumwa nimemuuliza unaweza kwenda nyumbani peke yako amenijibu hawezo na ameomba wewe umpeleke kwao"
baada ya mwalimu mkuu kuongea hayo nilimtazama sana swaumu ....
HUSIKOSE SEHEMU YA 11
DOWNLOAD APPLICATION YETU SASA KWA SIMULIZI NZURI ZA KUSISIMUA.
--https://drive.google.com/…/1qtYFz3rlGY7cOjkNj6LYq1HSeU…/view
SAMBAZA KWA WENGINE NA HUKO MBELE NDIO KUTAMU ZAIDI

No comments:

Post a Comment