Breaking

Saturday, February 22, 2020

UTAMU WA MAMA Sehemu Ya 41

UTAMU WA MAMA
MTUNZI: GODFREY GODSTAR
CONTACT: 0712730692
FB PAGE: Godstar_tz
SEHEMU YA 41
siku hiyo kwakweli ilikuwa ni mbaya kwangu,niliwakuta wanafunzi wapo mstarini,wakati naingia tu getini nikakutana na mwalimu wa zamu wa wiki hiyo alikuwa ni mwalimu kambona.
#ENDELEA NAYO
"masumbuko hadi wewe leo umechelewa!,hahahha wala sikuachi,aya nyie wote muliochelewa sogeeni hapa sehemu moja"
dah nikasema mwenyewe ndani ya moyo kwamba leo nimeyakanyaga,maana huyu mwalimu achapi ila anabutua na fimbo zake akikuchapa basi jua kabisa ni maumivu ya wiki nzima.
tulikaa pale huku tukisubiria tupewe adhabu ila kabla ya kupewa adhabu alikuja mwanafunzi mmoja akamsalimia mwalimu kambona.
"mwalimu samahani nimetumwa na mwalimu mkuu anamuhitaji masumbuko"
"oooh anamuhitaji wa nini kamwambie anasubiria adhabu yake amechelewa atakuja"
yule mwanafunzi baada ya kuambiwa hivyo aliondoka,mwalimu akaanza kutuchapa wakati tumebakia wachache yule mwanafunzi alikuja tena.
"mwalimu samahani tena,mwalimu mkuu amesema anamuhitaji asahivi ana kesi kubwa sana"
mwalimu akaniruhusu niende kwa mwalimu mkuu ila sasa hofu nyingine ikawa imetawala ndani ya moyo wangu,nikawa najiuliza nimefanya kosa gani kwa mwalimu mkuu,nimeokoka kwa mwalimu kambona sasa naenda kukutana na balaa la madame mwalimu mkuu.
wakati nakaribia lango la ofisi ya mwalimu mkuu alitokea dada mkuu swaumu.
"hahahahahahhahahahahahaha"
swaumu aliangua kicheko kikubwa sana hadi nikapatwa na mshangao,huku maswali yakiwa yamejaa kichwani mwangu,kuna nini leo maana siku imekuwa mbaya kwangu dah.
"masu ndio umefanya nini?,sasa nenda ukajibu kwa mwalimu mkuu maana umeyakanyaga mwenyewe"
daah nilizidi kuvurugwa akili,jasho likaanza kunitiririka,woga ulinizidi,basi swaumu alinishika mkono na moja kwa moja tukaingia ofisini kwa mwalimu,duuh nilikutana uso kwa uso na mwalimu.
"madame huyu hapa nishamleta"
"oooh vizuri,masumbuko mwanangu,vizuri sana......."
USIKOSE SEHEMU YA 42 YA HADITHI HII TAMU YA KUSISIMUA YA UTAMU WA MAMA LAZIMA UJUE KWANINI UTAMU WA MAMA.
DOWNLOAD APPLICATION YETU SASA KWA SIMULIZI NZURI ZA KUSISIMUA.
👉https://play.google.com/store/apps/details?id=com.godstarapp
SAMBAZA KWA WENGINE NA HUKO MBELE NDIO KUTAMU ZAIDI

No comments:

Post a Comment