Breaking

Tuesday, February 18, 2020

Watu 20 Wafariki Baada ya Kukanyagana Wakati Wakipokea Msaada
Wanawake 15 na Watoto 5 wamepoteza maisha baada ya kukanyangana wakati wakipokea msaada wa chakula, mavazi na fedha katika Mji wa Diffa, Kusini Mashariki mwa Niger

Inaelezwa kuwa, maelfu ya watu, wengi wao wakiwa wakimbizi, walisikia kuhusu msaada huo na kujitokeza kwa wingi jambo lililopelekea vurugu kuanza na watu kukanyangana

Mbali na vifo hivyo, watu wengine 10 wamejeruhiwa katika tukio hilo

Inadaiwa kuwa mara nyingi walengwa wa misaada hiyo hutuma wawakilishi kuipokea kwa niaba yao lakini hali ilikuwa tofauti wakati huu na waliamua kuja wenyewe

Mji huo una wakazi takriban 120,000, wengi wao wakiwa wamekimbia mashambulizi yanayofanywa na Wanamgambo wa Boko Haram, Kaskazini Mashariki mwa Nigeria.


No comments:

Post a Comment