Breaking

Tuesday, February 18, 2020

Watu 24 Akiwemo Askofu Wauawa Wakiwa Kwenye Misa


Shambulizi la silaha lililofanywa katika kanisa huko nchini Burkina Faso limesababisha vifo vya watu 24.

Kwa mujibu wa vyanzo vya habari vya nchini humo watu wasiofahamika waliokuwa na silaha walivamia kanisa katika kijiji cha Pansi, jimbo la Yagha,wakati misa ya Jumapili na kufanya shambulizi hilo la kinyama.

Kiongozi wa eneo la Sahel, Albay Binbasi Salfo Kabore alisema watu 24 akiwemo askofu wa kanisa waliuawa hapo hapo kwenye tukio hilo.

Watu 18 waliojeruhiwa kwenye tukio hilo wamepelekwa katika hospitali mbalimbali kwa ajili ya matibabu.

Katika nchi hiyo, watu zaidi ya 700 wameuawa katika  miaka 4 ya hivi karibuni kutokana na mashambulzi ya kigaidi huku watu watu zaidi ya  270 elfu wakiyakimbia makazi yao.

No comments:

Post a Comment