Breaking

Sunday, March 1, 2020

Acha Tabia Hizi..Haziendani na Utanashati.....

Mdau wa JamiiForums ameelezea baadhi ya tabia ambazo mtu akizifanya mbele ya Umma zinaondoa utanashati wake na kumshusha hadhi kabisa. Ameshauri Watu kuacha tabia hizo

Mdau amewashauri watu kuacha kutoa uchafu puani kwa vidole vyao maana pua ina bakteria wengi sana na badala yake watumie kitambaa. Pia, ameshauri kuacha kujishika sehemu za siri ndani ya nguo hata kama zinawasha na ikitokea unawashwa jikunie kwa nje ya nguo

Ameshauri pia kuacha kupenga kamasi kwa mikono mitupu na badala yake hakikisha unakuwa na kitambaa maalumu. Lakini pia ameshauri kunika nguo zako za ndani kwenye jua la kutosha na pia nawa maji ukitoka chooni kwa haja ndogo au kubwa

Amedai kuwa Muungwana yeyote anakuwa na kitambaa cha kujifutia jasho ukijiona unatembea bila ya kitambaa wewe ni mchafu. Mwisho ameshauri kuwa hakikisha makalio yako unayapaka mafuta, hasa wanaume ambao kwa asilimia kubwa hawapaki mafuta

HIZI HABARI ZA HIVI ZINAPATIKANA GODSTAR ONLINE >>BONYEZA HAPA KUDOWNLOAD APP YA GODSTAR ONLINE

No comments:

Post a Comment