Breaking

Saturday, March 21, 2020

China yasema Trump anajaribu kuhamisha lawama ya mripuko wa Covid-19


China imemshtumu rais wa Marekani Donald Trump leo kwa kujaribu kuhamisha lawama ya mripuko wa janga la Covid-19 duniani katika mzozo unaozidi kati ya mataifa hayo mawili.

Trump alidai jana Alhamisi kwamba dunia inalipa gharama kubwa kutokana na ukosefu wa uwazi wa China kuhusu mripuko huo ulipoanza katika mji wa katikati wa Wuhan mwishoni mwa mwaka uliopita.

China imekosolewa kwa kuzuwia taarifa na kuwaadhibu watoa taarifa katika hatua za mwanzo za mripuko huo.

Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Geng Shuang amesema baadhi ya watu katika upande wa Marekani wanajaribu kunyanyapaa mapambano ya China dhidi ya janga hilo na kuhamishia lawama kwa taifa hilo.

Amesema mkakati huo unapuuzia juhudi kubwa za kujitolea kwa watu wa China kulinda afya na usalama wa binadamu na unachafua mchango mkubwa wa China kwa afya ya umma ulimwenguni.

HIZI HABARI ZA HIVI ZINAPATIKANA GODSTAR ONLINE >>BONYEZA HAPA KUDOWNLOAD APP YA GODSTAR ONLINE

No comments:

Post a Comment