Breaking

Saturday, March 21, 2020

Dalili 6 Kuashiria Upo Kwenye Uhusiano Wa Kimapenzi Na Mtu Asiye Sahihi
Kumpata mtu sahihi wa kuwa nae kwenye uhusiano wa kimpenzi kwa watu wengi ni changamoto kubwa ambayo huhusisha kujaribu na kushindwa. Hii ina maana kuwa, njia bora ya kuweza kujua kama mtu ni sahihi kwako, ni hadi pale utakapokuwa naye kwenye uhusiano. Njia inaweza ikaonekana sio sahihi lakini ni njia ambayo itakupa majibu ya uhakika zaidi.
Ukigombana na mwenza wake mnapokuwa katika uhusiano wa kimapenzi, haimaanishi kwamba si mtu sahihi kwako, kwa sababu hakuna watu waliopo kwenye uhusiano ambao hawakwaruzani. Lakini kikubwa unahitaji jicho la tatu la kuuchunguza ugomvi huo ili kuweza kuelewa zaidi.
Unapokuwa kwenye uhusiano na mtu, na ukaona ishara hizi sita. Kwa asilimia kubwa zitakuwa zinakuonesha kwamba upo kwenye uhusiano na mtu ambaye si sahihi na unapaswa kuchukua hatua haraka.
1. Unakerwa na unakuwa na hasira dhidi yake
Kama ilivyoelezwa awali, ni jambo la kawaida kwa wapenzi kukwazana na kupishana kauli, lakini unapoanza kukereka na kuwa na hasiri juu ya vitu vidogo vidogo ambavyo mwanzo havikuwa sababu, fahamu kuna tatizo mahali.
Ukiona unakera na vitu vidogo ambavyo hata wakati mwingine havina msingi ambavyo pia hawezi kuvirekebisha, hiyo ni ishara kuwa uhusiano wenu hautafika mbali.
2. Kutupiana lawama
Inapofikia hatua kwamba hamuwezi kukaa chini na mkazungumza mambo yakaenda mbele, kila mkizungumza ni kurushiana lawama, ni kugombana na kuanza kutafuta mchawi ni nani, huenda huyo uliye naye si wako.
Kila ukikaa na kufikiri kwanini uhusiano wenu hauko sawa, unaona mwenzako ndio tatizo na yeye anaona wewe ndio tatizo, kunakuwa na mchezo wa kubebeshana lawama kwa kila baya linalotokea, chukua hatua za haraka.
3. Hakuna vitu vinavyofanana
Inapofika hatua hukumbuki au hufahamu tena vitu ambavyo kwa pamoja mnavipenda na vinawaunganisha ujue uhusiano wako upo kwenye mashaka. Kila unapopendekeza mfanya jambo mfano kwenda sinema, kula chakula au kutemba anaonekana hapendezwi au kuvutia na chochote unachosema, kuna shida.
Huenda mlikuwa na mvuto mkubwa mwanzoni mwa uhusiano wenu, lakini kufikia hatua hiyo inaonesha hamna kitu kinachoweza kwenda mbele tena.
4. Unatumia nguvu kubwa kuimarisha uhusiano
Haimaanishi kuwa mambo kwenye uhusiano wenu yatakuwa mteremko kwamba hutahitaji kutumia nguvu na muda wwako kuhakikisha mnakwenda sawa. Kinachosisitizwa hapa ni kwamba, unapoona kwamba wewe pekee ndio unatumia nguvu kuhakikisha kwamba uhusiano wenu unaendelea kuwepo, na mwenzako hajali au haoni jitihana unazozifanya, ondoka.
Uhusiano ulio bora kwako hautakufanya wewe kuwa mtu ambaye hujielewi, bali utakusaidia kuyafikia malengo yako na kuwa mtu uliyetamani kuwa.
Uhusiano unaokufanya unafanya mambo ambayo yanakufanya hata usijitambue wewe mwenyewe ili tu uhusiano udumu, huo sio sahihi kwako.
5. Unatamani kuwa na mtu mwingine
Unaweza usiwe unachepuka na mtu mwingine, lakini kwenye akili yako una kila mara unaona kuwa uliyenaye hakufai na kwamba huchoki kutamani kuwa na mtu mwingine.
Kila mnapotoka nje ya nchi, au unapokuwa nje peke yako, macho yako hayabanduki kwenye macho ya wasichana au wanaume ambao unawaona ni bora kuliko uliye naye.
Unapoona kuwa unakosa furaha na uliyenaye na mara kwa mara unatamani kuwa na mtu mwingine, basi ujue uliyenaye pengine si sahihi.
6. Umeshakata tamaa
Uhusiano unapoelekea ukingoni, kuna kuwa na mambo mawili. Kama unasikia maumivu na kusikia kama nafsi yako haiko radhi kuondoka, hapo inaonesha kuwa bado una nafasi ya kutetea uhusiano wako. Lakini kama uhusiano wako kufikia mwisho hakukufanyi wewe kusikia kitu chochote kwenye mwili wako, paki vitu vyako ondoka.
Kila mmoja wenu ana haki ya kuwa na mpenzi ambaye atamfanya ajisikie vizuri, na kama mnaona kuwa kwa kuwa pamoja mnaikosa haki hiyo, ni vyema mkaondoka.
HIZI HABARI ZA HIVI ZINAPATIKANA GODSTAR ONLINE >>BONYEZA HAPA KUDOWNLOAD APP YA GODSTAR ONLINE

No comments:

Post a Comment