Breaking

Sunday, March 22, 2020

Dk. Ndugulile: Dawa ya Chloroquine haitibu Corona inapunguza makali


Naibu waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na watoto, Dk Faustine Ndugulile, amesema  sawa ya Chloroquine inapunguza ukali wa homa ya mapafu (Pneumonia).

Ndugulile ameandika ujumbe huo katika ukurasa wake wa Twitter wakati akitoa elimu ya virusi vya Corona.

“Pia kufupisha muda wa kuugua homa hiyo kwa wagonjwa wa Corona,” aliandika Dk Ndugulile.

Amesema kuwa dawa hiyo haiponyi bali inapunguza makali ya ugonjwa, hivyo wananchi waendelee kuchukua tahadhari ya kujikinga na Corona.
HIZI HABARI ZA HIVI ZINAPATIKANA GODSTAR ONLINE >>BONYEZA HAPA KUDOWNLOAD APP YA GODSTAR ONLINE

No comments:

Post a Comment