Wakili wa kujitegemea, Fatma Karume amemcharua Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kwa kitendo cha kumtangaza mtoto wa Freeman Mbowe kuwa ni mgonjwa wa Corona.
“@makonda-paul huna mamlaka ya kumtaja mgonjwa kwa jina,” aliandika Fatma Karume katika ukurasa wake wa twitter.
Aliongezea kuwa “Ilikuwa upeleke Ambulance kwenda kumchukua awekwe Quarantine na si kumtaja hadharani,” aliandika.
Fatma aliandika ujumbe huo baada ya kuona Makonda anamjibu Waziri wa afya jamii na maendeleo, jinsia, wazee na watoto kwa kudai yupo sahihi kwa asilimia 100 kutangaza kwa kuwa ni mwenyekiti wa usalama mkoa wa Dar es salaam
@makonda_paul Huna MAMLAKA ya kumtaja mgonjwa kwa jina. Ilikuwa upeleke AMBULANCE kwenda kumchukuwa awekwe QUARANTINE na si KUMTAJA hadharani.
58 people are talking about this
No comments:
Post a Comment