Breaking

Saturday, March 21, 2020

Hii Ndio Maana ya Kuning'iniza Viatu Juu ya Nyaya za Umeme

Ushwahi kuona viatu vimening'inizwa juu ya nyaya za umeme hapo mahali unapoishi au mahali popote ulipowahi kutembelea?
Je,unajua ina maana gani?
Usijali tupo hapa kukujuza yote haya.


Kitendo hiki kimetapakaa sana siku hizi za karibuni lakini wengi wetu hatujui maana halisi ya kitendo hiki,hakika kina maana nyinghi tofauti tofauti hivyo huwezi kutafsiri kwa jumla ya vitendo vyote kila mahali,ifuatayo ni oropdha ya maana hizo

01# HUWAKILISHA MAHALI PAUZWAPO DAWA ZA KULEVYA

Mara nyingi uonapo viatu vimening'inizwa juu ya nyaya za umeme maana yake eneo la karibu na hapo panauzwa dawa za kulevya.kwa mfano kuna gazeti moja la huko LOS ANGELES,CALIFORNIA lilieleza kuwa hofu ya wakazi wengi wa LOS ANGELES ni kuwa viatu hivyo huwakilisha maeneo yauzwapo dawa za kulevya.

02# HUFANYIKA KUTOKANA NA UKOROFI

Baadhi ya wahalifu walieleza ni kwanini kitendo hiki kinafanyika ,baadhi yao walieleza kuwa ni kutokana na ukorofi,yaani mtu mkorofi huweza kuiba viatu na kuvining'iniza juu ya nyaya za umeme ili yule alieibiwa kamwe asivipate viatu vyake.

03# KWA UPANDE WA WANAFUNZIKwa wanafunzi wao hufanya hivi katika kusherehekea kumaliza kwa muhula wa masomo,katika lusherehekea huko hutupa viatu.

04# KWA UPANDE WA WANAJESHI


Wao hutupa viatu kwenye vitu vyenye kukwea angani kama nyaya za umeme,miti na nyaya za simu.
Wanajeshi hutupa viatu kwa sababu mbili-

Ni kwa wale waliomaliza mafunzo maalum hawa hutupa viatu kusherehekea kumaliza mafunzo hayo.
Hutupa viatu mara baada ya kumaliza muda wao wa kuhudumu jeshini yaani kustaafu (sio wote hufanya hivi ila ni baadhi yao tu ndio hufanya hivi katika hali ya kusherehekea)


05# HUTUPA VIATU WAKIWA HAWAVIHITAJI

Sababu nyingine inayopelekea kuwapo kwa viatu hivi juu ya nyaya za umeme ni kwamba wengine wanatupa pindi wanapokuwa hawavihitaji tena viatu vyao.

06# MARA NYINGINE HUMAANISHA MTU AMEFARIKI

Kwa baadhi ya tamaduni wao hufanya hivi kuwakilisha kuwa kuna mtu amefariki mahala fulani,wao hutupa viatu kwenye miti na nyaya za umeme kwa wingi na sio pea moja.

07# KIUTAMADUNIWengine hufanya hivi kwa kuamini kuwa mpendwa wao aliefariki pindi roho yake itakaporejea basi itatembea juu juu na hata karibu na mbingu na pepo.
Na watu wengine wanaamini kuwa kuweka viatu juu ya mti au nyaya ya umeme nje karibu na nyumba wanazoishi huwaepusha na kuwaweka salama wao na mali zao dhidi madhara na vitisho vya nizimu
 mila nyingine zinaeleza kuwa kutungika viatu kwa mtyindo huo kunawafanya kuwa salama zaidi.


#POWERED_BY
GodstarOnline

HIZI HABARI ZA HIVI ZINAPATIKANA GODSTAR ONLINE >>BONYEZA HAPA KUDOWNLOAD APP YA GODSTAR ONLINE

No comments:

Post a Comment