Breaking

Tuesday, March 3, 2020

Huyu Ndio Nyoka Mwenyekasi zaidi na Mwenye Sumu Kali zaidi Duniani

#FAHAMU:Huyu ndio nyoka mwenyekasi zaidi na mwenye sumu kali zaidi duniani,Nyoka huyu ujulikana kama KOBOKO au Black Mamba.

hupatikana katika sehemu za Mashariki na Kusini mwa Afrika huishi katika Makazi yoyote ambayo hutoa joto na unyevunyevu.

Nyoka huyu akitaka kufanya shambulio hutanua kinywa chake na shingo yake na hutoa sauti kama ile ya tairi likiwa linatoa upepo.
Black mamba ana aina mbili ya sumu zinazozalishwa katika mwili wake moja ni huitwa (Neuro) hii huathiri mfumo wa neva na nyingine ni (Cardio-toxin) hii huathiri mfumo wa moyo na sumu hizi zinaweza kuua binadamu chini ya dakika 20.

Pia imethibitika kuwa matone mawili ya sumu yake yanaweza kuua lakini mbali na kiasi kikubwa cha sumu kali sana aliyonayo, Koboko hana ujanja mbele ya Nguchiro,Mbweha, na Nyegere.

HIZI HABARI ZA HIVI ZINAPATIKANA GODSTAR ONLINE >>BONYEZA HAPA KUDOWNLOAD APP YA GODSTAR ONLINE

No comments:

Post a Comment