Breaking

Monday, March 23, 2020

INAWEZEKANA: Bibi Mwenye Miaka 95 Apona Corona

Bibi mwenye umri wa miaka 95 raia wa Italia amepona ugonjwa wa corona baada ya kukutwa virusi vya ugonjwa huo mapema mwezi huu.

Alma Clara Corsini, (95) kutoka Modena, Italia alilazwa hospitalini tangu Machi 5, 2020
Wataalamu wa afya nchini Italia wamesema mwili wa mgonjwa huyo ulionyesha uwezo mkubwa wa kupambana na virusi hivyo.

Alma alipelekwa katika hospitali ya mkoa wa kaskazini mwa Pavullo Machi 5 baada ya kuonyesha dalili za virusi vya corona, ugonjwa ambao hadi sasa umegharimu idadi kubwa ya maisha ya raia wa nchi hiyo.

Alma aliliambia gazeti la Italia la Gazetta Di Modena kuwa hivi sasa yuko sawa. “Ndio, ndio, niko sawa. Walikuwa watu wazuri ambao walinitunza vizuri na sasa watanipeleka nyumbani kidogo.”
Wataalamu hospitalini hapo wamesema kuwa bibi huyo aliweza kupona bila 'tiba ya antiviral'- dawa ambazo hutolewa kwa mgonjwa kuwasaidia kupigana na maambukizi ya virusi.

Italia, ambayo ilitangaza kifo cha kwanza cha mgonjwa wa corona Februari, sasa ina vifo zaidi ya 5,000.

Jumapili, Italia ilipiga marufuku kusafiri ndani ya nchi hiyo katika jaribio lingine la kuzuia kuenea kwa virusi hivyo.

HIZI HABARI ZA HIVI ZINAPATIKANA GODSTAR ONLINE >>BONYEZA HAPA KUDOWNLOAD APP YA GODSTAR ONLINE

No comments:

Post a Comment