Breaking

Tuesday, March 24, 2020

Jack Wolper Atamani Kuzaa Mtoto, Ataja SIFA za Mwanaume Anayetaka Kuzaa Naye


Msanii wa filamu na mfanyabiashara Jacqueline Wolper, amekiri kusema anatamani kuwa na mtoto kwa sababu umri unaenda ila bado hajajua nani atakuwa Baba wa kuanzisha naye familia.

Msanii huyo ameyasema hayo kupitia video fupi aliyopost katika akaunti yake ya mtandao wa Instgram, ambapo amevitaja vigezo vya mwanaume anayemtaka.

"Nataka niwe na mtoto, unajua umri unakwenda lakini nani atakuwa ndiyo baba, vigezo namba 1 mpaka 4"

1. Asiwe tajiri

2. Awe mchapakazi ajue kazi na asichague kazi, hata nikimwambia leo tunaenda Kariakoo shimoni kuna deal ya nyanya zimetoka tukanunue, tuuze tupate pesa awe tayari kwa kifupi asiwe bishoo.

3. Awe ana hofu ya Mungu, asiwe anavuta sigara wala unga kilevi chochote ruksa, asiwe staa wa kabila lolote wala dini yoyote.

4. Awe msafi muda wote asiwe na mtoto umri miaka 30 na kuendelea, urefu ufupi uzuri siyo tatizo, muhimu vigezo uwe navyo haijalishi uwe mbaya au la, maana sipendi wanaume wazuri haijalishi una kazi au hauna, tutapambana na kazi yangu paka tuwe matajiri.

Hivi sasa Jacqueline Wolper anatajwa kuwa kwenye mahusiano na msanii wa HipHop hapa nchini Young Killer.


HIZI HABARI ZA HIVI ZINAPATIKANA GODSTAR ONLINE >>BONYEZA HAPA KUDOWNLOAD APP YA GODSTAR ONLINE

No comments:

Post a Comment