Breaking

Thursday, March 12, 2020

Kimenuka...Wawili Kortini kwa kufungua namba zilizofungwa na TCRA

Watu wawili wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu mkazi Kisutu wakikabiliwa na mashtaka matatu likiwemo la kujihusisha na kufungua Simu zilizofungwa na TCRA ili kubadili uhalisia wa IMEI namba.Wakisomewa mashtaka hayo na wakili wa serikali Esther Martin mbele ya Hakimu mkazi mwandamizi Augustina Mbando watu hao Abdul Nassor na Said Msangi ambao ni mafundi simu Kariakoo Dar es Salaam wanadaiwa Februari 27 mwaka huu walibadili namba tambulishi ya Simu aina ya Tekno.


Wawili hao pia wanadaiwa kubadili namba za simu tambulishi maarufu IMEI. Ikumbukwe kuwa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) ilifungia simu zote bandia au ambazo hazikufikia viwango vinavyo takiwa kutumika hapa nchini.

Source Azam Tv

HIZI HABARI ZA HIVI ZINAPATIKANA GODSTAR ONLINE >>BONYEZA HAPA KUDOWNLOAD APP YA GODSTAR ONLINE

No comments:

Post a Comment