Breaking

Saturday, March 14, 2020

Kisa Visa vya CORONA Kenya Nayo Yasitisha Shughuli za Soka


SHIRIKISHO la soka nchini Kenya (FKF) limeazimia kusimamisha shughuli zote rasmi za soka nchini humu baada ya uthibitisho wa kesi ya kwanza ya mwathirika wa virusi vya Corona nchini humo.

FKF tayari limesimamisha  mashindano yote rasmi ya vijana, mashindano ya wanawake ikiwemo ligi ya wanawake, Ligi Daraja la Kwanza  na Ligi Daraja la Pili.

Ligi Kuu ya soka nchini humo KPL itaendelea na ratiba yake wikiendi hii kwa mechi kadhaa kupigwa lakini bila ya uwepo wa mashabiki, huku agizo la kusimamisha michezo hiyo likitarajiwa kuanza kutekelezwa kuanzia Jumatatu, Machi 16.

Pia, katika kujihadhari na virusi hivyo, shirikisho limeziagiza klabu zote nchini humo kusitisha shughuli zote zinazohusisha mikusanyiko ya wachezaji, wafanyakazi wa klabu au mashabiki kama programu za mazoezi, mikutano na mikusanyiko ya mashabiki.

HIZI HABARI ZA HIVI ZINAPATIKANA GODSTAR ONLINE >>BONYEZA HAPA KUDOWNLOAD APP YA GODSTAR ONLINE

No comments:

Post a Comment