Breaking

Monday, March 23, 2020

Kocha wa Arsenal Mikel Arteta anasema 'amepona corona'

Mkufunzi wa klabu ya Arsenal Mikel Arteta anasema kuwa ''amepona kabisa'' coronavirus.

Mhispania huyo wa miaka 37,alikuwa mkufunzi wa kwanza wa ligi ya primia kupatikana na virusi vya corona Marchi 13.

Aliripotiwa kujihisi vibaya baada ya kutangamana na Evangelos Marinakis - mmiliki wa klabu ya Ugiriki ya Olympiakos, ambayo ilicheza na Arsenal katika ligi ya Europa Februari - kupatikana na coronavirus Machi 10.

Arteta anasema: "Iilimchukua siku tatu hadi nne kuanza kujihisi vyema, nikiwa na nguvu, nazo dalili zikapotea."

Akizungumza na kituo cha televisheni cha Kihispania cha La Sexta aliongeza kusema: "Najihisi vyema sasa. Nahisi nimepona."

Wachezaji wa Gunners walitarajiwa kurejea uwanjani kwa mazoezi sikiu ya Jumanne baada ya kukamilisha siku 14 ya kujitenga ilipobainika Arteta ameambukizwa virusi vya corona lakini mpango huo umeahirishwa.

"Kutokana na hali ilivyo sasa, tunafahamu itakuwa utepetevu mkubwa kuwaambia wachezaji warudi uwanjani wakati huu," ilisema taarifa kutoka kwa usimamizi kwa klabu hiyo ya London kaskazini.

"Kwahivyo kikosi chetu cha kwanza cha wanaume na wanawake pamoja na wachezaji katika chuo cha mafunzo watasalia nyumbani. Kaeni nyumbani muokoe maisha."

Wachezaji kadhaa wa Arsenal walijiweka karantini baada ya kupata taarifa ya Marinakis kuambukizwa virusi vya corona,wakati ambapo Gunners walikuwa wanajiandaa kukipiga dhidi ya Manchester City katika uwanja wa Etihad Machi 11.

Akizungumza siku ya Jumapili, Arteta aliongeza: "Baada ya mazoezi nikiwa ndani ya gari langu nilipokea simu kutoka kwa bodi ya wakurugenzi na waliniambia kuwa rais wa Olympiakos amepatikana na virusi vya corona na kwamba kila mmoja aliyekuwa karibu naye yuko katika hatari ya kupata maambukizi.

"Niliwaelezea kuwa binafsi sijihisi vyema na kuongezea kuwa hali sio shwari ikizingatiwa baadhi ya wachezaji walitangamana na muathiriwa .

"Tulikuwa na mechi dhidi Manchester City siku iliyofuata hali ambayo bilashaka ingeliweka watu wengi hatarini tusipochukua hatua yoyote.

"Kila mmoja aliyenikaribia hakuwa na budi kujitenga, na kutoka na hilo mechi iliahirishwa."

HIZI HABARI ZA HIVI ZINAPATIKANA GODSTAR ONLINE >>BONYEZA HAPA KUDOWNLOAD APP YA GODSTAR ONLINE

No comments:

Post a Comment