Breaking

Wednesday, March 18, 2020

Lema Amjibu DPP " Mimi Sikuogopi Nina Kesi Nyingi Mahakamani Unaweza Kushauri Chochote"

Zikiwa zimepita siku kadhaa tangu Mkurugenzi wa Mashtaka nchini (DPP), Biswalo Mganga, kuahidi kuwa atamchukulia hatua Mbunge wa Arusha Mjini Godbless Lema, kwa kuwa alitoa taarifa za uongo kuhusu mauaji ya watu 14 mkoani Singida, Mbunge huyo ametoa kauli zake pia.

Mbunge Lema amedai kuwa, DPP hana mamlaka ya kisheria ya kuita vyombo vya habari na kuanza kumhukumu hata kabla ya mahakama haijamhukumu.

"DPP alisema kuna jambo yeye na ofisi yake watajua watalifanya, kauli yangu ni moja kwako mimi sikuogopi, unaweza ukafanya chochote unachotaka kukifanya kwangu, nina kesi nyingi mahakamani unaweza kushauri chochote" amesema Lema.

HIZI HABARI ZA HIVI ZINAPATIKANA GODSTAR ONLINE >>BONYEZA HAPA KUDOWNLOAD APP YA GODSTAR ONLINE

No comments:

Post a Comment