Breaking

Tuesday, March 17, 2020

Magufuli Asimamisha Kazi Wahandisi 12, Amuonya Waziri
Rais Dkt. John Pombe Magufuli awasimamisha kazi wahandisi 12 wa wote 12 wa Wakala wa barabara nchini TANROADS Mkoa wa Morogoro na kuwapa onyo la mwisho Waziri wa Ujenzi, Mhandisi Isack Kamwelwe, Mtendaji Mkuu TANROADS, Mhandisi Patrick Mfugale na Mkurugenzi wa matengenezo wa wakala huo kwa uzembe uliosababisha kuvunjika kwa daraja la Kiegeya mkoani humo.

Magufuli amefanya uamuzi huo leo, Jumatatu, Machi 16, 2020 alipotembelea katika Daraja hilo kushuhudia nililvyokatika kwa mvua kubwa zinazoendelea kunyesha na kusababisha kukatika mawasiliano kati ya Dodoma na Morogoro.


“Sitaki kuona barabara ya mkoa au kuu imefungwa kwa sababu daraja limekatika, sitaki kusikia kwa TANROADS wote Tanzania nzima kwa sababu nafahamu fedha za kufanya ‘maintenance’ zipo, haiwezekani daraja mpaka likatike Engineer upo na fedha unazo. Kila barabara ikikatika katika mkoa yule Regional Manager ajihesabu hana kazi,” amesema Magufuli.

By KATUGA BOY.

HIZI HABARI ZA HIVI ZINAPATIKANA GODSTAR ONLINE >>BONYEZA HAPA KUDOWNLOAD APP YA GODSTAR ONLINE

No comments:

Post a Comment