Breaking

Monday, March 9, 2020

Manara Anyosha Mikono kwa Yanga "Wanasimba Wenzangu Tukubali Tumefungwa na Timu iliyocheza Vizuri Kuliko sie"


Ofisa habari wa simba sport club Haji Manara ameamua kuwapigia saruti watani wao wa jadi Yanga baada ya kukubari kichapo cha bao 1-0 mchezo uliopigwa jana uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. 

Kupitia ukrasa wake wa intargram ameonyesha busara kwa kuwapa pongezi watani wao kwa kusema walistahili ushindi na kuwataka wanasimba kuwa na uvumilivu na kujikita katika mchezo ujao. 

"Wanasimba wenzangu niwape salaam zangu fupi za kuwaomba kwanza tukubali tumepoteza mchezo wa jana kwa kufungwa na timu ilyocheza vzuri kuliko sie,,na tukubali hilo halibadiliki kwa sasa,,najua tumeumia ila hyo ndio football tuliyoichagua kuipenda,,kwa tamaduni zetu lazma tucharurwe kama ambavyo tungewacharura iwapo tungeshinda,,but life goes on ,,Muhimu kujipanga kwa mchezo unaofuata keshokutwa,,tusitoke ktk reli na sote tunajua ubingwa upo mikononi mwetu ,tusithubutu kumtafuta mchawi wala kulaumiana.


Wametufunga kihalali kabisa na ni haki yao kutamba!! 
But Insha'Allah tutachukua ubingwa"

No comments:

Post a Comment