Breaking

Saturday, March 28, 2020

Manne yanayomng’oa GSM Yanga haya hapa


HABARI mpya ni kwamba bado bilionea anayeipa kiburi Yanga, Ghalib Said Mohamed ameshikilia msimamo wake kutojihusisha na baadhi ya mambo ndani ya klabu hiyo huku akisisitiza kwamba amechoshwa na majungu. 

Lakini ishu nzito zaidi ni kwamba kikao cha siku mbili cha Kamati ya Utendaji ya Yanga kilichokutana Masaki Jijini Dar es Salaam, kilikuwa na mzozo wa aina yake na baadhi ya wajumbe wametishia kujiuzulu ili kumrejesha GSM ndani ya Yanga baada ya kuonekana kwamba wao ni tatizo. 

Ingawa viongozi wamekuwa wagumu kutoa tamko kwa yaliyojiri ndani, lakini Mwanaspoti limebaini kwamba kuna vigogo watatu ambao jana wajiweka pembeni kwani wamekuwa wakituhumiwa kwamba wao ndio walioibua ishu hiyo na kumtibua tajiri ambaye ameonekana kuleta furaha kwa mashabiki Jangwani. 

MANNE YANAYOMNG’OA YANGA 
Uchunguzi wa kina wa Mwanaspoti umebaini kwamba kuna mambo matano ambayo yamemkera GSM na kuamua kujiondoa Yanga. 

Kitendo cha GSM kumtumia mhamasishaji wa Yanga, Antonio Nugaz kuwagawia wachezaji posho mbalimbali za hamasa na vifuta jasho inasemekana imewakera baadhi ya wajumbe wa Kamati ya Utendaji ambao walitaka ishu hiyo ikabidhiwe kwa viongozi wafanye utaratibu wenyewe. Lakini tajiri akasema ule mkwanja anatoa kwa mapenzi yake na wala haipo kwenye makubaliano ndio maana anamtumia mtu wake na utaratibu wake. 

USAJILI 
Kitendo cha GSM kumalizana na mastaa kwa kuwasajili juu kwa juu na yenyewe imeleta maneno. 

Baadhi ya wajumbe wanataka apeleke fungu klabuni wao wamalizane na wachezaji hao ingawa tajiri huyo uchunguzi unaonyesha kwamba hupewa muongozo na viongozi wa juu na anachofanya ni kuwaita wachezaji kuelewana nao na kuwapa fungu lao. 

Baadhi ya wachezaji aliowasajili kwenye dirisha dogo ni Morrison, Haruna Niyonzima, Adeyun Saleh na Ditram Nchimbi pamoja na makocha wote. Lakini vilevile hawafurahishi kuona wachezaji wapya wakitambulishiwa ofisini kwa mdhamini huyo badala ya klabuni. Lakini tajiri akajibu kwamba alikuwa anatoa fedha wakati fulani lakini mambo yakawa yanaenda tofauti na matarajio yake. 

BIASHARA YA JEZI 
Habari zinasema kwamba kuna baadhi ya wadau ambao ishu ya GSM kushinda tenda ya kuuza jezi za Yanga iligusa masilahi yao ya kiuchumi, hivyo hawakufurahishwa kwa vile walishatengeneza mzigo wao ndio maana wakaanza maneno ya 
Hoja nyingine ya wanaompinga GSM ni kwamba ameonekana kuwa mbele zaidi kuliko viongozi wa wanachama na anaingilia majukumu mengi ambayo walipaswa kufanya wao kama kuandaa timu mpaka ishu za mechi huku wao wakiwa hawaonekani kabisa. 

UONGOZI UNASEMAJE? 
Mwenyekiti Dk. Mshindo Msolla alitangaza jana kwamba tayari uongozi wao umeijibu barua ya GSM ya Machi 24, hii ikiwa ni baada ya maamuzi ya pamoja ya kikao cha Kamati ya Utendaji, ambacho kiliwachukulia hatua za kinidhamu baadhi ya wajumbe wake.

HIZI HABARI ZA HIVI ZINAPATIKANA GODSTAR ONLINE >>BONYEZA HAPA KUDOWNLOAD APP YA GODSTAR ONLINE

No comments:

Post a Comment