Breaking

Friday, March 27, 2020

Marekani Yaongoza Maambukizi ya Corona, Yaipiku China

MAREKANI imeripoti jumla ya maambukizi 85,604 na kuwa nchi yenye maambukizi mengi zaidi ikiizidi China yenye maambukizi 81,340 na Italia yenye maambukizi 80,589.

Hata hivyo, Italia bado inaongoza kwa vifo vilivyotokana na #Covid_19, ikiwa imetangaza vifo 8,215 ikifuatiwa na Hispania yenye vifo 4,365 huku Marekani ikiwa na vifo 1,301 na China kuna vifo 3,292.

Huko Chicago katika Gereza la Cook County lenye wafungwa 5,400, wafungwa 24 wamepatikana na mambukizi ya virusi vya #corona baada ya wafungwa 89 kuonyesha dalili kama za mafua na kupimwa.

Aidha, Meya wa Los Angeles, Eric Garcetti, ameonya kuwa kwa namna maambukizi yanavyoongezeka, California yenye maambukizi 4,044 inaelekea kuwa New York huku New York yenye maambukizi 38,977 inaenda kuwa kama Italia.


HIZI HABARI ZA HIVI ZINAPATIKANA GODSTAR ONLINE >>BONYEZA HAPA KUDOWNLOAD APP YA GODSTAR ONLINE

No comments:

Post a Comment