Breaking

Wednesday, March 25, 2020

Mbowe Aeleza Mwanaye Alivyopata Corona "Hatustahili Kuchefuliwa na Kejeli za Makonda"


Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe amemuomba Rais Magufuli, kushirikisha wadau wengine nje ya Serikali ili kwa pamoja waweze kukabiliana na janga la Corona kwa kuwa lipo mlangoni kwa kila mtu kwani hata mwanaye umempata ndani ya nchi.

Mbowe aliyasema hayo kupitia taarifa ya familia yake kwa umma na Dunia nzima, wakati akieleza ni kwa namna gani mwanaye alivyopatwa na maambukizi ya Virusi vya Corona, ambapo amesema huu si wakati wa malumbano na njia pekee ya kulishinda janga hilo ni kulikubali na kulikabili.

"Hali ya Dudley sasa imeimarika, homa zimekwisha, bado yuko chini ya uangalizi maalum kwenye karantini, hatustahili kuchefuliwa na kejeli za Makonda, Rais wetu John Magufuli, unda timu ya kukusaidia na ushirikishe wadau wengine, wengi wako tayari kukusaidia CHADEMA tuko tayari kukusaidia na kulisaidia Taifa, siyo wakati wa kulumbana  huu" amesema Mbowe.

Aidha Mbowe ameongeza kuwa katika maisha, maandalizi hayajawahi kuwa hasara, bali hasara iliyo majuto ni kutokujiandaa na kupuuza yanayofanywa na walioyapitia kama zilivyo nchi zingine zilizoendelea.


HIZI HABARI ZA HIVI ZINAPATIKANA GODSTAR ONLINE >>BONYEZA HAPA KUDOWNLOAD APP YA GODSTAR ONLINE

No comments:

Post a Comment