Breaking

Saturday, March 28, 2020

Mbowe Afanya Mazungumzo na Profesa Lipumba Akiwa Karantini, Watume Ujumbe


Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi CUF, Profesa Ibrahim Lipumba amefanya mazungumzo na Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema ambaye kwa sasa yupo karantini kufuatiwa motto wake kukutwa na virusi vya Corona.

Lipumba alizungumza na Mbowe kwa njia ya simu wakati akiendelea na mahojiano na kituo kimoja cha Televisheni, Lipumba alitoa pole kwa Mbowe na kumpongeza kwa kauli zake kwa umma ambazo zimekuwa ni chachu ya mapamabano ya kuenea kwa virusi hivyo.

“Tunamuaombea kila la heri mwanao aweze kupona tunamuombea kwa mnyezi Mungu, ni mtihani wa Mungu lakini tunashuru wanafamilia wengine hamna,” Profesa Lipumba amemweleza Mbowe.

Kwa upande wake Mbowe amemshukuru Lipumba kwa kumjulia hali na kutoa wito kwa viongozi na wasio viongozi kutoa elimu sahihi juu ya ugonjwa huo huku akisisitiza kuwa sio wa kupuuzwa

HIZI HABARI ZA HIVI ZINAPATIKANA GODSTAR ONLINE >>BONYEZA HAPA KUDOWNLOAD APP YA GODSTAR ONLINE

No comments:

Post a Comment