Breaking

Friday, March 6, 2020

Meneja wa Diamond Achoka, Amtaka ao


Dar es Salaam. Wakati kitendawili cha kuachana kwa msanii Diamond Platnumz na mpenzi wake Tanasha Donna kikiwa hakijateguliwa, meneja wake, Mkubwa Fella amemshauri msanii huyo kuoa.

Mkubwa Fella ametoa ushauri huo leo Jumatano Machi, 5 2020 kupitia ukurasa wake wa Instagram kwa kuandika "Nafurahi kila hatua mwanangu Naseeb deni lako moja tu kwangu nalijua na unalijua mashahidi Sallam SK, Babu Tale, Mama Dangote (mama yake Diamond), Uowe."

Ni kutokana na ujumbe huo Mwananchi ilimtafuta Fella ambaye mbali ya kuwa meneja wa msanii huyo kutaka kujua kwa nini ameandika ujumbe huo kwa sasa na kama kuna uhusiano wowote na tetesi za Diamond kuachana na mpenzi wake.

Katika maelezo yake, Fella amesema suala la Diamond na Tanasha kuachana hana analolijua na kueleza kuwa amejikuta akiandika ujumbe huo kwa kuwa anaona umri wa msanii huyo kuoa umefika.

 "Diamond alipo kiumri anaruhusiwa kuoa, hivyo sipendezwi kuona mpaka sasa hana mke na analijua hilo kuwa ni jambo ambalo kila siku namsisitiza kulifanaya.


 "Kama vile haitoshi uwezo wa kuishi na mke anao na pia ni mtu ambaye kila analoliomba naona anafanikiwa, sasa anasubiri nini asioe na neema kwake zinamiminika kila uchwaa hata jana ni mashahidi mmeona alivyosaini dili jingine la ubalozi,"amesema Fella.


HIZI HABARI ZA HIVI ZINAPATIKANA GODSTAR ONLINE >>BONYEZA HAPA KUDOWNLOAD APP YA GODSTAR ONLINE

Alipoulizwa kuhusu ni mwanamke gani hasa angependa kuona Diamond anamuoa, Fella amesema yeyote tu ilimradi kumridhia na kuongeza kuwa kwake  kila  mwanamke anayemuona na msanii huyo kwake hana kipingamizi kwa kuwa ndio chaguo lake. 

HIZI HABARI ZA HIVI ZINAPATIKANA GODSTAR ONLINE >>BONYEZA HAPA KUDOWNLOAD APP YA GODSTAR ONLINE

No comments:

Post a Comment