Breaking

Saturday, March 28, 2020

Mfahamu Mwanaume Mwenye SURA Mbaya Tanzania Mwaka 1996 Ambaye Mpaka Leo Hakuna Mpinzani


Lilikuwa ni Shindano la Aina yake ambalo haijawahi tokea tena toka nchi yetu imepata uhuru. Lengo la Shindano ni kutamfuta mtu mwenye SURA MBAYA kuliko wote. Ilikuwa ni miaka ya 90 enzi hizo.

Walijitokeza washiriki wengi kwenye shindano hilo na baada ya mchakato wa mchujo walibaki washiriki watatu kwa ajili ya kushiriki fainali.

Washiriki hao kwa ajili ya fainali walikuwa ni MZEE JANGALA(pichani kulia), mwanamuziki REMMY ONGALA (katikati) na bwana mmoja anaitwa MASOUD (?) pichani kushoto.

Baada ya shindano la fainali bwana MASOUD akaibuka mshindi wa kwanza kama mtu mwenye SURA mbaya, wa pili akawa remmy ongala na wa tatu mzee jangala.

Hayati Dr. Remmy hakukubaliana na maamuzi ya majaji kumpa ushindi wa kwanza bwana Masoud kwani aliamini yeye ndiye alistahili kuwa mshindi wa kwanza hivyo akakata rufaa.

Rufaa ikasikilizwa, wachunguzi na majaji wakafuatilia historia na familia ya bwana Masoud ikaonekana na kuamriwa kwamba bwana Masoud anastahili ushindi wa kwanza kwani kwenye familia yao karibu wote wana sura mbaya,hadi dada zake. Tena ikaonekana yeye ana afadhali.

Hivyo rufaa ya Dr Remmy dhidi ya ushindi wa Bwana "MASOUD SURA MBAYA" kama mtu mwenye sura mbaya kuliko wote ikatupiliwa mbali. Katika Rufaa Yake Dk Remmy Alidai Masoud Ni Aliugua Ukoma Sio Sura Yake! Ahaaaa. Bwana Masoud akakabidhiwa zawadi yake,kama sikosei ilikuwa ni pesa taslimu Tsh 50000/=. _
Ila Dr remmy hadi anafariki dunia hakukubaliana na ushindi wa bwana Masoud .

Nakumbuka shindano hili liliandikwa sana Radio Tanzania na Magazetini. Ilikuwa ni burudani kwelikweli!๐Ÿ˜‚๐Ÿ™Œ

Kupitia Shindano Hilo Mshindi MASOUD SURA MBAYA alipata Umaarufu Uliopelekea Kuwahi Kuwa Kwenye Video Ya Wimbo Wa Juma Nature "Hakuna Kulala"

Wanaume wa siku hizi mnajiedit mitandaoni ilimuonekane wazuri wajinga nyinyi๐Ÿ˜ค

HIZI HABARI ZA HIVI ZINAPATIKANA GODSTAR ONLINE >>BONYEZA HAPA KUDOWNLOAD APP YA GODSTAR ONLINE

No comments:

Post a Comment