Breaking

Tuesday, March 17, 2020

Mgonjwa wa Corona wa Tanzania Azungumzia Afya yake "Nataka Nijipodoe"Mgonjwa aliyetambulika na Corona, Isabella Mwampamba (46) ambaye amelazwa katika hospitali ya Mount Meru mkoani Arusha hatimaye asimulia afya yake na kueleza anaendelea vizuri.

Alisema afya yake inaendelea vizuri waondoe hofu kwani anaoga mwenyewe na kupaka mafuta, hivyo wajulisheni na wengine katika mitandao ya kijamii.

“Mimi naendelea vizuri kabisa namshukuru Mungu waambie katika magroup yenu dada Isabela ni mzima nataka baadaye nikishaoga nijipake mafuta nijipodoe vizuri, nijirembe vizuri nianze kuongea na kuwajibu watu ,”


Juzi Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu akizungumza na waandishi wa habari alisema kuna mgonjwa mmoja wa corona ambaye anaendelea na matibabu katika hospitali ya Mount Meru.

Waziri Mwalimu aliwatoa hofu wananchi kwamba tayari serikali inaendelea kuchunguza hatua madhubuti kuhakikisha ugonjwa huo unadhibitiwa usisambae nchini.

HIZI HABARI ZA HIVI ZINAPATIKANA GODSTAR ONLINE >>BONYEZA HAPA KUDOWNLOAD APP YA GODSTAR ONLINE

No comments:

Post a Comment