Breaking

Saturday, March 21, 2020

Mo atao msaada kusaidia mapambano ya Corona asema ni mwanzo tu

Bilionea maarufu nchini Tanzania Mohammed Dewji (Mo) amesema kampuni yake punde itaanza kutengeneza sanitaizer ikiwa ni sehemu ya kampuni hiyo kusaidia mapambano dhidi ya ugonjwa virusi vya Corona.

Mo ameeleza hayo kupitia ukurasa wake wa Twitter na kueleza kuwa amewapa kazi watu wake kuangalia na namna gani kampuni hiyo inaweza ikaisaidia jamii katika mapambano haya ya Corona.

Hata hivyo siku moja baadaye Mo aliposti picha ya taasisi yake ikijenga eneo la kunawia mkiono katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili, na kusema kuwa hiyo ni hataua ya kwanza wanendelea kuangalia namna nyingine ya kusaidia.

HIZI HABARI ZA HIVI ZINAPATIKANA GODSTAR ONLINE >>BONYEZA HAPA KUDOWNLOAD APP YA GODSTAR ONLINE

No comments:

Post a Comment