Breaking

Saturday, March 28, 2020

‘Mpenzi Wangu Chioma ana Virusi vya CORONA, ‘ Msanii Davido Atangaza


Msanii maarufu kutoka Nigeria, Davido ametangaza kuwa mpenziwe, Chioma amepimwa na kupatikana na virusi vya COVID-19.

Akitangaza habari hizo kupitia ukurasa wake wa Instagram, Davido alisema kuwa wawili hao pamoja na marafiki na watu wengine 31 wa karibu wamekuwa katika pilkapilka za safari za nje ya nchi.

Ni kwa sababu hiyo waliamua kujitolea na kupimwa mnamo Machi 25 ili kubaini hali yao.

Alisema kuwa yeye alirudi nyumbani hivi punde baada ya show zake za Marekani kutatizwa na virusi hivi na mpenziwe Chioma alikuwa amezuru mji wa London pamoja na mwanao.

Hata hivyo baada ya kupimwa, Chioma ndiye aliyepatikana na virusi hivyo, lakini mwanao yuko salama salmini.

Davido anasema kuwa licha ya wawili hao kutoonesha dalili zozote za COVID-19, waliona ni vyema kujitenga kwa siku 14 ili kusaidia kuzuia usambazaji wa virusi hivyo.

Hata hivyo, alizidi kuwahimiza mashabiki wak ekubakia nyumbani na  kuchunga afya yao ,huku akiwashukuru kwa maombi yao na kuendelea kumshika mkono.

Soma ujumbe wake;

Hey everyone! I came back recently from America after postponing my tour. My fiance Chioma also came back from Lodon recently with our baby. We had no symptoms and still both feel perfectly fine but because of our recent travel history we decided to take ourselves and our close associates we’ve come in recent contact with for the COVID-19 test on the 25th of March. Davido alisema.

Aliendelea,

Unfortunately, my fiance’s results came back positive while all 31 others tested have come back negative including our baby. We are however doing perfectly fine and she is even still yet to show any symptoms whatsoever. She is now being quarantined and I have also gone ito full self isolation for the minimum 14 days. I want to use this opportunity to thank you all for your endless love and prayers in advance and to urge everyone to please stay at home as we control the spread of this virus! Together we can beat this! Love, D.


HIZI HABARI ZA HIVI ZINAPATIKANA GODSTAR ONLINE >>BONYEZA HAPA KUDOWNLOAD APP YA GODSTAR ONLINE

No comments:

Post a Comment