Breaking

Saturday, March 14, 2020

Mshambuliaji wa Chelsea Aliyekuwa na Virusi vya Corona Afya yake yaanza Kuimarika


MSHAMBULIAJI wa Chelsea, Callum Hudson-Odoi amesema kuwa kwa sasa anaendelea vizuri baada ya kufuata kanuni za afya ili kupona virusi vya Corona.

Nyota huyo mwenye miaka 19 alikutwa na virusi vya Corona baada ya kufanyiwa vipimo kutokana na kuhisiwa kwamba huenda ameathirika.

 "Naendelea vizuri na ninashukuru kwa wote ambao mmekuwa mkitaka kunijulia hali juu ya afya yangu, ninachokifanya kwa sasa ni kufuata kanuni za afya hii itakuwa rahisi kwangu kurejea kwenye ubora," amesema.

Kutokana na mlipuko wa Corona, Ligi Kuu ya England imesimashwa kwa muda na inatarajiwa kurejea  Aprili 3.

HIZI HABARI ZA HIVI ZINAPATIKANA GODSTAR ONLINE >>BONYEZA HAPA KUDOWNLOAD APP YA GODSTAR ONLINE

No comments:

Post a Comment