Breaking

Saturday, March 28, 2020

Msigwa Asema Hoteli zote za Serena zimefungwa kwa Sababu ya CORONA...Amtupia Kijembe Waziri Kigwangalla


Mbunge wa Iringa mjini (Chadema), Mchungaji Peter Msigwa, amesema hoteli kubwa za Serena zimefungwa kutokana na ugonjwa wa virusi vya Corona.

“Hizi Serena ni hoteli kubwa zimefungwa. Hoteli moja unaweza kuwa na wafanyakazi zaidi ya 200 porini huko hakuna kabisa mtalii,” aliandika Mchungaji Msigwa katika ukurasa wake wa twitter.

Mchungaji Msigwa ni Waziri kivuli wa Maliasili na Utalii aliendelea kuandika kuwa

“@HKigwangalla liambie taiga what is up? Mr minister, don’t printed as if nothing is happening!,”

Katika tangazo lililitolewa na uongozi wa Serena hotel umeeleza kufunga hoteli zake za kitalii, Safari Lodge and camps na Hotel- Resorts kwa ajili ya kujikinga na Corona hadi Juni 15, 2020.

HIZI HABARI ZA HIVI ZINAPATIKANA GODSTAR ONLINE >>BONYEZA HAPA KUDOWNLOAD APP YA GODSTAR ONLINE

No comments:

Post a Comment