Breaking

Thursday, March 12, 2020

Mtayarishaji wa Filamu Weinstein Ahukumiwa Kifungo cha Miaka 23 Jela Kisa Ngono

Mtayarishaji wa zamani wa filamu Harvey Weinstein amehukumiwa kifungo cha miaka 23 jela kwa kufanya mashabulio ya kingono na ubakaji.

Weinstein mwenye umri wa miaka 67, ambaye aliwasili mahakamani jana akiwa katika kiti cha kusukumwa na alipelekwa hospitali baada ya kulalamika kuhusu maumivu ya kifua masaa kadhaa baada ya kesi hiyo kusikilizwa, anaweza kumaliza maisha yake yote akiwa jela.

Weinstein amehukumiwa mwezi uliopita kwa kumbaka msichana ambaye alikuwa anataka kuwa mcheza sinema mjini New York mwaka 2013 na kulazimisha kufanya ngono ya mgomoni na msaidizi wa zamani wa utengenezeji vipindi vya televisheni na filamu, Mimi Haleyi, nyumbani kwake mwaka 2006.

Hukumu hiyo ni ya kwanza ya uhalifu miongoni mwa madai kadhaa ambayo mtayarishaji huyo wa filamu aliyepata tuzo ya Oscar akitumia uwezo wake kuwashawishi wanawake, matumizi ya nguvu kufanya ngono ama kuwabughudhi wanawake na kisha kuwanyamazisha.

Wanawake wote ambao Weinstein amekutikana na hatia ya kuwatumilia nguvu kingono wameiambia mahakama juu ya uharibifu alioufanya kwao, na nguvu waliohisi wanayo wakati wakitoa ushahidi dhidi yake.

HIZI HABARI ZA HIVI ZINAPATIKANA GODSTAR ONLINE >>BONYEZA HAPA KUDOWNLOAD APP YA GODSTAR ONLINE

No comments:

Post a Comment