Breaking

Thursday, March 19, 2020

Mtu Mmoja Auawa na Raia Kwa Kudhaniwa Ana Corona Virus


Polisi huko Kwale Kenya wanakisaka kikundi cha watu ambacho kimemuua kijana Hezron Kotin eneo la Kibundani baada ya kumtuhumu kuwa na #COVID19

Kamanda wa Polisi wa Kaunti ndogo ya Msambweni, Nehemia Bitok alisema kijana huyo alikuwa akitembea kutoka kwa eneo la kunywa na aliingia kwenye kundi la vijana ambao walianza kupiga kelele kuwa ana ugonjwa

Vijana hao walishambulia mtu huyo wakiwa na silaha na kupelekea kifo chake. Kamanda wa Polisi alisema, waligundua jeraha kubwa kichwani mwake na kumkimbiza katika Hospitali ya Rufaa ya Msambweni

Polisi wameonya raia dhidi ya kuchukua Sheria mikononi mwao au kutoa madai ya uongo wakati Nchi inachukua hatua za kupambana na janga la #COVID19

Kaunti ya Kwale imeanza kutoa mafunzo kwa Maafisa wa Afya juu ya kushughulikia kuenea kwa virusi hivyo. Afisa Mkuu wa Afya, Juma Mbete alisema wameweka vituo vitano vya kutengwa katika Kaunti zote tano.


HIZI HABARI ZA HIVI ZINAPATIKANA GODSTAR ONLINE >>BONYEZA HAPA KUDOWNLOAD APP YA GODSTAR ONLINE

No comments:

Post a Comment