Breaking

Saturday, March 21, 2020

Mtu mwenye umri wa miaka 55 auawa kikatili na watu wasiojulikana Tanga


Na Rebeca Duwe, Tanga.

Mtu mmoja mwenye umri 55 mkazi wa Magaoni A, jijini Tanga aliyepotea kwa siku sita amekutwa ameuwawa na watu  wasiojulikana Kisha kufukiwa nyuma ya nyumbani kwake.

Akielezea tukio Hilo Mwenyekiti wa mtaa wa Magaoni A,kata ya magaoni mkoani Tanga Hassani Musa amesema mtu huyo anafahamika kwa jina la  Rogers Mwavya alipotea tangu tarehe 14march na kupatikana 19 March,2020 akiwa ameuwawa na kufukiwa mita 50 nyuma ya nyumba yake,huku ng'ombe wake kumi na baadhi ya mali zake zikiwa hazijulikani zimekwenda wapi na mchungaji wake ajulikani halipo.

Mwenyekiti Rajabu amesema katika eneo Hilo kumezoeleka kutokea matukio Kama haya zaidi ya 3 kinyama hivyo anaiomba serikali ya mkoa kusaidia kuimarisha ulinzi ili watu wasiendelee kuuawa kinyama.

Kwa upande Wake dada wa marehemu Fedh Mwavya amesema anasikitishwa na tukio hilo na anahisi mchunga ng'ombe wa kaka yake ndiyo amefanya tukio hilo hivyo analiomba jeshi la polisi lifanye uchunguzi juu ya tukio hilo.

Naye Diwani ya kati ya Magaoni jijini Tanga Muhamedi Rajabu amesema matukio hayo yanaendelea kutokea siku baada ya siku katika eneo ambalo alijaendelezwa la kampuni tanzu ya shirika la reli nchini (RAHACO)kwa Sasa nipoli hivyo mamlaka husika ujitahdi kuimarisha ulinzi na kukomesha matukio hayo.

Sambamba na hayo Jeshi la polisi linawataka wakazi wa mkoa wa Tanga kutoa ushirikiano ili kufanikisha kukamatwa kwa watumiwa wa mauaji ya Rogers   Mwavya yaliyotokea hivi karibuni.

Kauli hiyo imetolewa na Kaimu kamanda wa polisi mkoa wa Tanga Leons Rwegasira wakati akizungumzia suzla hilo.

Amesema ushiriki wa wananchi utasaidia kufanikisha kuwakamatwa kwa watuhumiwa waliyotenda tukio hilo la kinyama,Kama wataogopa kufika polisi basi wawatumie wenyeviti wa mtaa,madiwani na viongozi wa dini ili kuwafichua wahusika waliyotenda watukio hilo.

Kamanda Rwegasira ameeleza jinsi tulio hilo la mauaji lilivyofanyika ambapo marehemu Rogers Mwavya alipigwa na kitu butu kichwa kisha kufukiwa kwenye shimo nyuma ya nyumba yake,mpaka Sasa hakuna mtu aliyekamatwa juu ya Tukio hilo.

HIZI HABARI ZA HIVI ZINAPATIKANA GODSTAR ONLINE >>BONYEZA HAPA KUDOWNLOAD APP YA GODSTAR ONLINE

No comments:

Post a Comment