Breaking

Tuesday, March 17, 2020

Muna Love "Shetani wa Mitandaoni Alitaka Kuniyumbisha ila Nikamuaibisha"


Mtumishi wa Mungu Muna Love ameiambia EATV & EA Radio Digital, kwamba tukio lake la kutangaza kujitoa mitandaoni na taarifa za kubadilisha dini na kuolewa na Muisilam lilikuwa ni lakupitiwa na shetani.


Muna Love amesema wakati anatangaza kujitoa mitandaoni kisha kurejea baada ya siku mbili, alikuwa anajaribiwa na shetani ambaye alikuwa anamdanganya na kumyumbisha lakini amemshindwa.

"Suala la kujitoa mitandoni niliona shetani alikuwa anataka kuniyumbisha na kunidanganya, nikaona hapana acha nimuaibishe yeye nirudi, naweza kuishi bila mitandao lakini mwisho wa siku ina faida na mimi kwenye kutangaza biashara zangu" ameeleza Muna Love.
HIZI HABARI ZA HIVI ZINAPATIKANA GODSTAR ONLINE >>BONYEZA HAPA KUDOWNLOAD APP YA GODSTAR ONLINE
Aidha akizungumzia tukio la kubadilisha dini na kuolewa na ndoa ya kiislam, amesema, "Kwenye suala hilo nitakuja kuongea na waandishi wa habari  ili kuwaeleza ukweli wa tukio hilo na waliyoyaona, lakini wakae wakijua mimi ni mwanamke kuolewa na kujifungua watoto ni haki yangu, wakati wa Mungu ni wakati sahihi"

No comments:

Post a Comment