Breaking

Saturday, March 7, 2020

Nilimuacha Kimasihara, Sasa Hivi Najuta

Sasa hivi ni miaka mitatu imepita tangu nimuache kiutani utani mwanamke alienipenda kwa dhati.
Naomi mwanamke ambae aliweka malengo ya milenia kwangu ni vile mimi nikajivimbisha kichwa na kujiona mimi ndio mimi ,star sana .


Nakumbuka kila asubuhi before hajaenda chuo , alikuwa anapitia ghetto ananipikia chai ,na kunipa show kisha anaenda shule..
Alihakikisha napendeza muda wote maana alinifuria nguo, ghetto liling'aa muda wote.kipindi hicho yuko kachuo fulani anasomea kozi ya nursing,alisema akimaliza chuo tutaoana,

Ikafika kipindi amemaliza chuo yupo anasikilizia apate kazi,akaja kwangu kukaa huku anafanya harakati za kutafuta kazi, kadri siku zinavyozidi kusonga mbele ndivyo nilivyozidi kumuona wa kawaida.

Ilipita miezi kama mitatu hivi naishi naye sasa nikawa nimemchoka.nikaenda kwa jamaa yangu nikamuelezea, kwamba yule demu nimemchoka nitumie mbinu gani kumtoa.
Jamaa yangu akaniambia mbona mwanamke mzuri sana,anaheshima,kwanini unataka ufanye hivyo,
Nikamwambia nimemchoka,pili sihitaji,kuoa kwa wakati huu.

Jamaa yangu alisikitika sana,akasema wenzako wanaombea wapate mwanamke kama wako, wamebakia wachache sana.

Siku hiyo naomi alipigiwa simu na kaka yake, anahitajika aende alishafayiwa mpango wa kazi.
Akaniaga vizuri na kusema atanipa updates za kila kinachoendelea huko,

Asubuhi yake nikiwa nampeleka stand kwaajili ya safari,nilionekana nafurahi sana,hADI akaniuliza mbona nina furaha sana, inaonekana nafurahi kuondoka kwake, nikamwambia Mimi nafurahi kupata kwake kazi,

Basi kilichofuata ni kabadirisha namba,akawa akija namkimbia kimbia,kumficha na kumkwepa kidizaini.

Baada ya kukimbia kimbia sana aliandika barua,akamuchia yule jamaa yangu.

Kwenye barua akasema,,"najua unaninifichama kama umeamua kuniacha si uniambie tu ili nielewe nifanye mambo mengine kuliko kujipotezea muda"

Ilipita miaka miwili hatujawasiliana ila mimi nilisikiaga kuwa anafanya kazi huko irembura hospitali..wala sikuwahi kumtafuta.

Bwana mwaka huu nimeonana naye mtoto ameng'aa kapendeza kawaka sana.ameniambia kashaolewa tena kwa ndoa na ana mtoto wa miezi kama mitatu hivi.nilitetemeka na kuondoka haraka sana.

HIZI HABARI ZA HIVI ZINAPATIKANA GODSTAR ONLINE >>BONYEZA HAPA KUDOWNLOAD APP YA GODSTAR ONLINE

Wadau nilimuacha kimasihara sasa hivi najuta sana haipiti sekunde sijamfikiria yeye,naumia wanawake wengine wapo kimaslahi zaidi,ila naomi ame change sana kawa mzuri sana, tofauti na alivyokuwa zamani,,

Nifanye nini niache kumuwaza kila saa.

HIZI HABARI ZA HIVI ZINAPATIKANA GODSTAR ONLINE >>BONYEZA HAPA KUDOWNLOAD APP YA GODSTAR ONLINE

No comments:

Post a Comment