Breaking

Saturday, March 28, 2020

Queen Darleen Atangazia Wadada Kuwa Diamond Platnumz yuko Single..Changamkia Fursa

Msanii wa Bongo Diamond Platinumz yuko Single na wanadada wanafaa kukumbuka hilo wakati wote. Hayo  yamesemwa na dadake msanii huyo Queen Darleen ambaye amesema kakake bado ni mtanashati na hivyo basi hafai kujifungia.
Queen aliyasema hayo katika ujumbe  alioambatanisha na picha ya kakake katika akaunti yake ya instagram. Huenda sasa ni rasmi kwamba  Simba kweli kaachana na Tanasha Donna kwa sababu dadake anawafungilia wanadada wengine milango katika maisha ya kaka yake.


Katika posti hi ya Insta, dadake mwingine wa Diamond, Esma naye alicheka kwa bezo akisema kwamba huenda akina dada wanamuogopa Kaka yao. Huenda familia ya Diamond ipo nyuma yake kuhusu maamuzi anayofanya ya kuwatema vipusa wote wanaoingia katika maisha yake. Huku wanadada walioathirika wakilalama, dada zake na mamake wameonekana kulichukulia suala zima kama sarakasi na drama!


HIZI HABARI ZA HIVI ZINAPATIKANA GODSTAR ONLINE >>BONYEZA HAPA KUDOWNLOAD APP YA GODSTAR ONLINE

No comments:

Post a Comment