Breaking

Saturday, March 14, 2020

Rais Magufuli Afunguka Kuhusu CORONA..Atoa Tamko Hili Hapa

Amesema mpaka sasa Tanzania bado haijapata mgonjwa wa #coronavirus ila nchi haiwezi kujiweka pembeni lazima kuchukua tahadhari kwasababu ugonjwa huu unaua kwa haraka sana

Pia, amemuagiza Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi John Kijazi kupunguza kutoa vibali kwa watendaji kusafiri nje ya nchi na kuwataka wananchi wapunguze safari na kuchukua tahadhari dhidi ya #coronavirus

Rais ameyasema haya leo wakati akizindua Karakana ya matengenezo ya magari na mafunzo ya ufundi ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), Lugalo, Dar ambayo imejengwa kwa ufadhili wa Ujerumani kwa gharama ya Tsh. Bilioni 8.5

HIZI HABARI ZA HIVI ZINAPATIKANA GODSTAR ONLINE >>BONYEZA HAPA KUDOWNLOAD APP YA GODSTAR ONLINE

No comments:

Post a Comment