Breaking

Thursday, March 26, 2020

Rais wa DRC atangaza hali ya dharura nchini kote kupambana na virusi vya Corona

Rais Felix Tshisekedi wa Jamhuri ya Kidemokraisa ya Kongo DRC ametangaza hali ya dharura nchini kote, ikiwa ni juhudi za kupambana na virusi vya Corona.

Rais Tshisekedi amesema, uamuzi huo umetokana na hatari kubwa ya virusi hivyo, na kutangaza hatua nyingine kadhaa ikiwemo kusimamisha safari zote za kuingia na kutoka katika mji mkuu wa Kinshasa na mikoa mingine ili kuuweka mji huo kwenye karantini.

Rais Tshisekedi amelitaka jeshi la polisi na vikosi vya usalama kufanya dora ya pamoja ili kuhakikisha hatua hizo zinatekelezwa kwa manufaa ya watu wote.

Pia rais Tshisekedi ametangaza kufunga mipaka na kuruhusu malori, meli na ndege za mizigo muhimu tu kuingia nchini humo.

Mpaka sasa, kuna jumla ya kesi 48 za maambukizi ya virusi vya Corona nchini DRC.


HIZI HABARI ZA HIVI ZINAPATIKANA GODSTAR ONLINE >>BONYEZA HAPA KUDOWNLOAD APP YA GODSTAR ONLINE

No comments:

Post a Comment