Breaking

Tuesday, March 17, 2020

Sababu za Lulu Diva Mwili Wake Kuwa Biashara

Mrembo katika muziki wa BongoFleva Lulu Diva amesema anapenda urembo na mwili wake ni sehemu moja wapo ya biashara zake katika harakati zake za kutafuta pesa na maisha.

Akipiga stori na EATV & EA Radio Digital, amesema mwili wake ni biashara kwa sababu watu wengi wanamshabikia na watu wengi wanampenda kutokana na kujirusharusha kwenye video.

"Mwili wangu biashara kwa sababu naweza nikaitwa mahali kwa sababu ya muonekano wangu wanavyoniona na wakanilipa pesa, wengine wanapenda jinsi nilivyo na ninavyojirusharusha kwenye video halafu msanii anatakiwa awe na muonekano kuanzia mavazi hadi maisha yake nje ya muziki" Lulu Diva 

Aidha msanii huyo ameongeza kusema yeye  anapenda sana urembo na kama mtu hatampenda kwenye muziki basi atampenda kupitia muonekano wake ambao unapatikana katika mwili wake.

HIZI HABARI ZA HIVI ZINAPATIKANA GODSTAR ONLINE >>BONYEZA HAPA KUDOWNLOAD APP YA GODSTAR ONLINE

No comments:

Post a Comment