Breaking

Thursday, March 19, 2020

Sarah wa Harmo Yamkuta, Aoga Mvua ya Matusi


MCHUMBA wa msanii Rajab Abdul ‘Harmonize’ au Harmo, Sarah Michelotti, yamemkuta kwa kuogeshwa mvua ya matusi, kilichomponza nguo aliyovaa. Stori ipo hapa.

 

Mwishoni mwa wiki iliyopita kwenye uzinduzi wa Albam ya Harmo iitwayo Afro East, ndani ya Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar, Sarah alitinga na gauni lenye mpasuo matata huku kifuani likiachia sehemu kubwa ya ‘chakula cha mtoto’ jambo lililowafanya wengi kupigwa na butwaa.

 

Baada ya shoo hiyo ya kufa mtu kumalizika, ni kama ukurasa mpya wa marejeo ya matukio ulifunguliwa na gumzo likahamia kwenye gauni alilovaa Sarah siku hiyo.

Kwenye mitandao ya kijamii, hali ya hewa ilichafuka kwa baadhi ya watu kuposti picha hiyo sambamba na maneno mazito yasiyoandikika gazetini.

 

Hoja ilikuwa ni kwamba Sarah hakupaswa kuvaa nguo hiyo na kujitokeza mbele ya wageni waalikwa wenye heshima waliohudhuria shoo hiyo.

Baadhi ya watu wenye heshima waliohudhuria shoo hiyo ni Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Harrison Mwakyembe, Rais Mstaafu Jakaya Kikwete na Naibu Spika, Tulia Akson.

 

“Inaonesha Konde hakumwambia mama kuwa hapa si Ulaya kwa watu kukaa utupu, kwani… (maneno yasiyofaa),” komenti moja ilisomeka kwenye ukurasa wa Instagram wa msanii maarufu Bongo, aliyeposti picha mbalimbali za shoo hiyo ya Afro East.

 

Sarah mwenyewe hakuonesha kujutia vazi lake, kwani hata yeye aliweka picha hiyo na kuonesha kufurahia alivyotokelezea.

Hali haikuwa hivyo kwa wengine, kwani pekuapekua ya mwandishi wetu kwenye mitandao ya kijamii, ilionesha kuwa wengi hawakufurahishwa na vazi hilo na hivyo kumtolea maneno makali Sarah.

 

Hata hivyo, kama ilivyo kwa mkosaji kutetewa na wakili, ndivyo ilivyokuwa kwa Sarah kwani baadhi ya watu waliwajia juu waliokuwa wakimshambulia na kuwaambia “Waache ushamba.”

“Wabongo bwana, kila kitu kukosoa, hivi mlitaka avae ovaroli ndiyo aende kwenye shoo?” Mwanamke mmoja alitupia komenti yake kwenye ukurasa wa Instagram.

 

Official_halima_suba alitupia imoji za kufa mtu kwenye ukurasa wa Sarah wa Instagram, akionesha kuvutiwa na picha iliyolalamikiwa.

Sarah na Harmo wamekuwa katika uhusiano wa kimapenzi kwa takriban miaka minne na kuwafanya wawe miongoni mwa wachumba wazoefu!


HIZI HABARI ZA HIVI ZINAPATIKANA GODSTAR ONLINE >>BONYEZA HAPA KUDOWNLOAD APP YA GODSTAR ONLINE

No comments:

Post a Comment