Breaking

Saturday, March 14, 2020

Staa wa Uganda Spice Diana Atua Bongo Kufanya Collabo Kubwa na Harmonize

MSANII wa muziki wa kizazi kipya kutoka nchini Uganda, Namukwaya Hajara Diana, maarufu kwa jina la ‘Spice Diana’ ametua Bongo kwa ajili ya Tour na kujitangaza kimuziki huku pia akisaka connections kwa wasanii wa Bongo Fleva ili aweze kushirikiana nao na kuu-push muziki wake.

Akipiga stori katika mahojiano na Kipindi cha Bongo 255 kupitia +255 Global Radio, Spice ambaye tayari ameachia dude lake liitwalo Jangu Ondabe alilomshirikisha rapa maarufu wa kike Bongo, Rosery Robert ‘Rosa Ree’, amesema kuwa yuko tayari kufanya kolabo na wasanii wengine wakali hapa nchini, kwani anauelewa vizuri muziki wa Bongo ulivyo na mashabiki wengi Barani Afrika.
“Niseme kwamba kwa sasa niko tayari kufanya kazi na wasanii wa hapa Tanzania kwani tayari nimeshafanya kolabo na Rosa Ree na kwa sasa natazamia kufanya kazi na msanii Harmonize pamoja na kufanya matamasha,” amesema Spice Diana mwenye shahada ya uandisi.
Spice Diana amesema ipo changamoto katika muziki wao, hasa kutokana na kutokuwepo kwa mamlaka husika ya kiserikali ambayo ingeweza kusimamia muziki nchini Uganda kama ilivyo kwa hapa nchini japo mipango imeanza ya kuwepo kwa mamlaka hiyo.

HIZI HABARI ZA HIVI ZINAPATIKANA GODSTAR ONLINE >>BONYEZA HAPA KUDOWNLOAD APP YA GODSTAR ONLINE

No comments:

Post a Comment