Breaking

Sunday, March 29, 2020

Usiogope Kuambiwa Unajipendekeza Sana, Ki Kubwa Jipendekeze Kwa Malengo

Siku zote huwa kuna watu ambao kazi yao kubwa ni kama mawakala wa shetani kwa hiyo huwaga wanatumia mbinu mbalimbali kukudhoofisha pale ambapo wanaona kuna dalili ya wewe kupiga hatua flani.

Na wengi wanaweza kukuambia hili neno UNAJIPENDEKEZA sio kwamba kweli wana maanisha hapana wanasema hivyo kwa sababu huenda mtu uliye naye karibu nao wanatamani wangekuwa na nafasi hiyo sasa ili kujikinga wanatumia mgongo wa neno KUJIPENDEKEZA.

Siku zote katika maisha ili ufanikiwe unahitaji kuwa karibu na watu waliofanikiwa na ili uwe karibu na watu waliofanikiwa lazima ujenge ukaribu nao sana ili nao wapate nafasi ya kukujua ili waweze kukusaidia pale ambapo kuna jambo unahitaji.

Neno UNAJIPENDEKEZA litakuwa baya sana pale ambapo utakuwa unajiweka karibu na watu ili kuharibia watu flani jambo ambalo sio zuri hata kidogo ila kama unajipendekeza kwa sababu kuna mambo yako unataka yafanikiwe bila kuathiri mtu mwingine basi usitie hofu kabisa.

Msingi mkubwa wa watu waliofanikiwa walijiweka karibu sana na wale waliofanikiwa na wangekuwa wanaogopa kujiweka karibu na watu hao kwa woga wa kuambia wanajipendekeza huenda mpaka leo wasingefika walipofika.

HIZI HABARI ZA HIVI ZINAPATIKANA GODSTAR ONLINE >>BONYEZA HAPA KUDOWNLOAD APP YA GODSTAR ONLINE

No comments:

Post a Comment