Breaking

Saturday, March 14, 2020

VIRUSI VYA CORONA: Mambo muhimu ya kuzingatia kuepuka, hatua za kuchukua


Ni virusi vipya vilivyosababishwa na aina nyingine ya virusi vya aina hii, kama ile ya mwaka 2003 (SARS-CoV) na 2013 (CIDRAP News). Kwakuwa hivi viligundulika mwaka 2019 vilipewa jina la Covid-19. Vilitokana na wanyama na vilianzia Wuhan, China.

Dalili za kuwa na maambukizi ya Virusi vya Corona

Virusi vinaweza kusababisha tatizo la mapafu. Pia, kukohoa, kuwa na homa, uchovu, maumivu ya misuli na kupata matatizo ya upumuaji. Hali ikiwa mbaya baadhi ya viungo vinaweza kushindwa kufanya kazi.

Dalili zinaweza kuonekana kati ya siku 1-14.

Virusi vinaweza kusambaa kutoka kwa mtu mmoja hadi mwingine, ambao wamesogeleana kwa umbali wa hadi futi 3.

Je kuna tiba?

Dawa zilizopo hivi sasa haziwezi kuponya bali humpa mgonjwa nafuu. Matibabu hufanyika kwa kuzingatia dalili zilizopo. Kupona au kupata nafuu kunategemea zaidi uimara wa kinga za mwili za muathirika.

Unapaswa kufanya nini unapohisi una Virusi vya Corona? ‘Usikimbilie hospitalini’

Unapojisikia dalili za kuwa na Virusi vya Corona, tafadhali usikimbie kwenda hospitalini, badala yake unashauriwa kufanya yafuatayo:

Baki nyumbani kwako na ujitenge na wanafamilia wako iwezekanavyo;
Piga simu/ Omba msaada maalum wa kitabibu ukieleza ukweli kuwa unahisi una Virusi vya Corona;
Epuka kushikana na mtu mwingine au kukaribiana na mtu mwingine.

 Jinsi ya kuepuka Virusi vya Corona:

Usimshike au kukaa karibu na mtu mwenye dalili hata moja ya Virusi vya Corona iliyoelezwa hapo juu, hasa kama anatoka nchi zilizoathirika;
Kaa umbali usiopungua futi 3 kutoka kwa mtu mwenye dalili, mfano anayepiga chafya;
Epuka kushika mdomo, macho na pua. Hii ni kwa sababu mikono hushika sehemu nyingi na inaweza kubeba virusi vya Corona;
Osha mikono yako kwa maji safi na sabuni, jifute mikono kwa uhakika pande zote hadi ikauke;
Hakikisha unafuatilia kwa ukaribu taarifa kuhusu Virusi vya Corona katika eneo/nchi yako.

HIZI HABARI ZA HIVI ZINAPATIKANA GODSTAR ONLINE >>BONYEZA HAPA KUDOWNLOAD APP YA GODSTAR ONLINE

No comments:

Post a Comment