Breaking

Saturday, March 14, 2020

Virusi Vya Corona Vyatua Nchi Jirani Ya Rwanda


Rwanda imethibitisha kisa chake cha kwanza cha virusi vya Corona (COVID-19). Raia wa India aliyewasili nchini humo kutoka Mumbai, India, Machi 8, 2020 amethibitishwa kuwa na virusi vya corona.

Kulingana na wizara ya afya, mgonjwa huyo hakuwa na dalili zozote za virusi vya Corona wakati anawasili nchini Rwanda na alijipeleka mwenyewe kwenye kituo cha afya Machi 13, ambapo alifanyiwa vipimo mara moja.

Kwa sasa anaendelea na matibabu, hali yake imeimarika na ametengwa na wagonjwa wengine. Wote aliokuwa na mgonjwa huyo wanaendelea kutafutwa katika juhudi za kuudhibiti ugonjwa huo

HIZI HABARI ZA HIVI ZINAPATIKANA GODSTAR ONLINE >>BONYEZA HAPA KUDOWNLOAD APP YA GODSTAR ONLINE

No comments:

Post a Comment